Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.). Mara
baada ya kuwasilisha nakala hizo Mhe. Mahiga na Balozi Kazungu walipata fursa ya kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya hususan kwenye sekta za biashara, uchumi na elimu. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai, 2018. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.