Monday, November 19, 2018

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania, Perth pamoja na Balozi wa Kenya nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Konseli wa Heshima wa Tanzania kwenye Jimbo la Perth nchini Australia, Bw. Didier Murcia alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba, 2018 kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Naibu Waziri  pamoja na kumweleza utekelezaji wa majukumu yake katika kuiwakilisha Tanzania, Perth. 

Ujumbe uliofuatana na Bw. Murcia. Kutoka kushoto ni Bw. James Chialo na Bw. Thierry Murcia kutoka Kampuni ya Ndovu Resources ya jijini Dar es Salaam

Bw. Murcia akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao

Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri, Bw. Charles Faini.



..........................Mkutano kati ya Naibu Waziri na Balozi wa Kenya nchini


Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba 2018. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia Balozi Kazungu alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Naibu Waziri kuhusu Mkutano wa Kimataifa kuhusu  Rasilimali Endelevu za Majini utakalofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018

Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini (kushoto) akiwa na Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Kazungu ambao hawapo pichani

Mhe. Balozi Kazungu akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao

Mhe. Balozi Kazungu akimkabidhi Mhe. Dkt. Ndumbaro moja ya nyaraka kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Rasilimali Endelevu za Majini utakaofanyika nchini Kenya.

Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Balozi Kazungu mara baada ya mazungumzo kati yao

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.