TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nafasi za masomo na ajira
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa za
masomo na ajira zinazotolewa na wadau mbalimbali duniani. Fursa zilizopokelewa
mwezi Machi 2019 ni kama ifuatavyo:
i.
Mafunzo ya Shahada ya Uzamili yanayotolewa
na Chuo Kikuu cha British nchini Misri (British University – Egypt) kwa kipindi
cha mwaka wa masomo 2019/2020. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia, na maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti, http://www.bue.edu.eg/;
ii.
Mafunzo ya Shahada ya Kwanza na Uzamili
yanayotolewa na Taasisi ya Elimu ya Urusi (Russian Education Institute)
kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020 na 2020/2021. Fursa hizi
zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Maelezo ya namna ya kuomba fursa hizo
yanapatikana katika Wizara zinazoratibu mafunzo hayo. Mwisho wa kufanya maombi
kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ni tarehe 25 Machi 2019 na tarehe 25 Juni 2020
kwa mwaka wa masomo 2020/2021;
iii.
Mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika
fani ya Usuluhisihi katika Mchakato wa kutafuta Amani (Mediation in Peace
Processes) yatakayotolewa nchini Uswisi katika kipindi cha mwaka wa masomo
2019/2021. Maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao kupitia
tovuti, http://www.mas-mediation.ethz.ch/. Mwisho wa kufanya maombi
ni tarehe 21 Aprili 2019;
NAFASI ZA AJIRA
iv.
Nafasi ya ajira ya Afisa Tathmini
(Evaluation Officer, P-3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi
ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition
of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika
tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-officer-industry-p-3_11.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Machi 2019; na
v.
Nafasi ya ajira ya Afisa Usalama wa
Masuala ya Habari (Information Security Officer, P – 3) katika Sekretarieti ya
Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the
Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya
kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-information-
security-officer-industry-p-3_18.aspx. Mwisho wa kutuma
maombi ni tarehe 26 Machi 2019.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
13 Machi
2019
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.