Tanzania inashiriki
katika Mkutano wa Mwaka kwa Nchi Wanachama wa KIMBERLEY PROCESSING
SCHEME, unaofanyika Jijini New Delhi nchini India. Ujumbe wa Tanzania
katika mkutano huo unaongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Mhe.
Stanslaus Nyongo. Mkutano huo unahusu nchi
wazalishaji wa Madini ya Almasi na udhibiti wa biashara ya
almasi duniani. Ushiriki wa
Tanzania katika mkutano huo unalenga katika kupata uzoefu
kutoka nchi nyingine zinazofanya vizuri katika biashara ya Madini hayo ghali duniani.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.