Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge
amekabidhiwa Ofisi rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji
K. Mnyepe kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06 Februari, 2020. Kabla ya uteuzi huo
Balozi Kanali Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol).
Aidha, Balozi Ibuge anachukua
nafasi ya Dkt. Faraji K. Mnyepe ambaye alihamishwa wizara kwa kuteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Dkt. Mnyepe
amechukua nafasi ya Dkt. Frolens Turuka ambaye amestaafu.
|
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akipokea baadhi ya nyaraka
za Ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam. Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimpa mkono aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe mara baada ya makabidhiano
rasmi ya Ofisi.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Ramadhani Mwinyi baada ya kumtembelea ofisini kwake
leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
|
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb) akiwa na Katibu Mkuu mpya wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert
A. Ibuge alipomtembelea Ofisini kwake leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar es Salaam
|
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.