Mkutano
wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi
ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Makatibu Wakuu/ Maafisa
Waandamizi umefanyika Jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video
Conferencing).
Mhimili
wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC unaongozwa na mfumo
wa Utatu (Troika) ambapo kwa sasa Mwenyekiti ni Zimbabwe, mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 26 Juni 2020 chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa
wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye
dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi na
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC.
Pamoja
na mambo mengine mkutano umepokea na kujadili agenda zinazohusu masuala ya
Siasa, Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa SADC.
Mkutano
wa leo umehudhuriwa na nchi wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini,
Botswana, DRC, Eswatini,
Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Asasi
ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni moja ya mihimili ya SADC
inayosimamia masuala ya Usirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda.
Mhimili huu unatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mkataba wa uanzishwaji wa
SADC wa mwaka 1992 na Itifaki ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na
Usalama ya SADC ya mwaka 2001.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge (katikati), kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi, Dkt. Faraji Mnyepe , mwisho kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Christopher Kadio wakifuatilia mkutano huo kwa njia ya video conference, Jijini Dar es salaam
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na
baadhi ya Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam
Mkutano ukiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.