Nchi za NORDIC ambazo ni Norway, Sweden, Finland na
Dernmark zimeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha kuwa
Tanzania inasonga mbele katika maendeleo yake kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya wiki ya Nordic
jijini Dar es Salaam, Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen amesema
kuwa nchi za Nordic zimeadhimisha wiki ya Nordic nchini Tanzania na zimejadili
masuala ya malengo ya maendeleo endelevu ambapo pamoja na mambo mengine, wametumia
wiki ya Nordic kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Nordic na
Tanzania.
"Wiki ya Nordic inatoa fursa ya kushirikiana na
kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii, kisiasa na kichumi pamoja na kupata
uzoefu wa maendeleo kutoka kwa kila mmoja wetu," Amesema Balozi Jacobsen.
Ameongeza kuwa, nchi za Nordic zimejidhatiti kufanya
kazi kwa karibu na Tanzania ili kuhakikisha kuwa Tanzania inasonga mbele katika
maendeleo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea mara baada ya kukabidiwa mpira ulioandikwa malengo 17 ya maendeleo endelevu ikiwa ni ishara ya kuhamasisha maendeleo ya Tanzania, amesema kuwa mpira huo ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi za Nordic.
"Ushirikiano wetu (Tanzania) na nchi za Nordic
ni wa muda mrefu kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru. Tumekuwa tukifurahia ushirikiano
wetu na nchi za Nordic na umekuwa ukimarika kila wakati, ni matumaini yetu sisi
kama serikali kuwa uhusiano utaendelea kuimarika zaidi," amesema Dkt.
Ndumbaro
Mwezi Novemba 2019, ulifanyika Mkutano wa Mawaziri
wa Mambo ya nje wa Afrika na Nordic, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano
huo uzikutanisha nchi za Afrika na Nordic na kutoa fursa ya kujadili masuala mbalimbali
yakiwemo, elimu, kilimo biashara na uwekezaji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwaelezea jambo Mabalozi wa nchini za Nordic |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na mabalozi wa nchini
za Nordic wakiwa
wameshikilia mpira ulioandikwa malengo 17 ya maendeleo endelevu
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.