Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Meja Generali (Mst.) Anselm Shigongo Bahati akifanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Giza Power kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya pande mbili. Kampuni hiyo inamiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za umeme kwa matumizi mbalimbali. Kadhalika, Mhe. Balozi Bahati alitembelea kiwanda hicho na kujionea uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho na kujadili na uongozi wa kiwanda hicho kuhusu kuja kuwekeza Tanzania. Kiwanda cha Giza Power kinafanya biashara ya nyaya za umeme na nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.