Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na
Mwakilishi katika Umoja wa Ulaya, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga akiwasilisha Hati
za Utambulisho kwa Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Mhe. Ursula
von der Leyen katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Makao Makuu
ya Umoja huo jijini Brussels, Ubelgiji tarehe 30 Julai 2020.
Wakizungumza baada ya kukamilika kwa
makabidhiano hayo viongozi hao waliazimia kudumisha na kuongeza maeneo mapya ya
ushirikiano mzuri uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 baina ya Serikali ya Tanzania
na Umoja wa Ulaya.
Kadhalika, Mhe. Nyamanga alieleza
Tanzania na Umoja wa Ulaya zimekuwa na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote
mbili hususan katika eneo la ubia wa maendeleo kwenye sekta za kilimo, miundombinu,
elimu, nishati, afya na mazingira. Hivyo, ushirikiano huo pia umehamasisha
uwekezaji, biashara na kutembeleana baina ya watu wa pande zote na kuzidi
kuongeza fursa kwa wananchi wake.
Tanzania na Umoja wa Ulaya pia
zinashirikiana katika mikakati mbalimbali ya kutafuta na kudumisha amani,
usalama na utulivu katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu, barani Afrika na
duniani kwa ujumla. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.