Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine Eng. Mlote alitoa taarifa fupi ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya Jumuiya ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazoiunganisha nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nishati na Vituo vya Kutoa Huduma Pamoja Mipakani (OSBPs)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote wakiwa katika mazungumzo. Wengine kutoka kulia ni Balozi Stephen P. Mbundi Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama na Hangi Mgaka, Afisa Mambo ya Nje
Mazungumzo yakiendelea
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Kamugisha Kazaura, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen P. Mbundi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.