Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.
Hafla
ya kuwasilisha hati za utambulisho imefanyika Ikulu jijini Nairobi ambapo
pamoja na mambo mengine, Rais Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa
Tanzania nchini Kenya, Mhe. Balozi Simbachawene.
Balozi
Simbachawene amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa ataendelea kuboresha mahusiano ya nchi hizo mbili za Tanzania na Kenya, kukuza biashara baina ya nchi hizo kwa kuboresha diplomasia ya uchumi kwa ujumla wake.
Rais
wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta akiwa tayari kupokea hati ya utambulisho kutoka
kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene
Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.