RAIS
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Magufuli na Rais wa Jamhuri
ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus Chakwera wameweka jiwe la msingi katika kituo
kipya cha mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es Salaam
Kabla
ya kuweka jiwe la msingi, Rais Dkt.Magufuli ametoa maagizo, kwa waziri wa Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika
kabla ya tarehe 30 Novemba 2020, vinginevyo mkandarasi atakatwa Pesa kwa kuchelewesha
mradi.
Kituo
hicho kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba mabasi 1,000 na teksi 280 kwa siku,
Pia kutakuwa na maeneo ya bodaboda na bajaji na na eneo la mamalishe na
babalishe.
Mbali
na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha mabasi mbezi Luis, Rais Chakwera pia
ametembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na mradi wa Ujenzi
wa Reli ya Kisasa (SGR), Kampuni ya Huduma za Kontena Bandarini (TICTS), Kituo
cha Mizigo cha Malawi (Malawi Cargo Center) pamoja na Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na mgeni wake Rais wa
Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera mara baada ya
kumpokea katika eneo la ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi
Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakiwa wamesimama huku wakiimba nyimbo za
Taifa za mataifa yote mawili kabla ya kuanza rasmi kwa shughuli ya uwekaji wa
jiwe la msingi katika maradi wa ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akipongezana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus
McCarthy Chakwera mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la maradi wa ujenzi wa
stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi
akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy
Chakwera kuongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy
Chakwera mradi wa ujezi wa Reli ya Kisasa (SGR) wakati alipotembelea mradi huo Jijini Dar es Salaam |
|
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus
McCarthy Chakwera akiongea na wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza wakati
alipotembelea mradi wa ujenzi wa SGR jijini Dar es Salaam. Kushoto mwa Rais Chakwera ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa akifuatiwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi. |
|
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus
McCarthy Chakwera pamoja na mkewe Mama Monica Chakwera wakipokea zawadi kutoka
kwa uongozi wa Kituo
cha Mizigo cha Malawi (Malawi Cargo Center) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa SGR
jijini Dar es Salaam |
|
Rais
wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa, Dkt. Lazarus Chakwera pamoja na mkewe
Monica
Chakwera wakimsikiliza Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika
bandari ya Dar es salaam (TICTS), Bw. Horace Hui mara baada ya kutembelea
kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam Rais
wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa, Dkt. Lazarus Chakwera akiongea na wananchi pamoja na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati alipotembela Bandari ya Dar es
Salaam leo jijini Dar es Salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.