Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi
Na Nelson Kessy, Gaborone-Botswana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC Organ Troika (Botswana, Malawi
na Zimbabwe), na nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa
Mataifa, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye Kikosi cha
Umoja wa Mataifa nchini DRC utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2020, mjini
Gaborone, Botswana.
Akithibitisha kuhusu
ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ujumbe wa
Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa anamwakilisha Mhe. Rais.
Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, mkutano huu utatanguliwa
na mkutano wa Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama na kufuatiwa na mkutano wa Dharura wa Kamati ya
Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 26 Novemba 2020.
"Pamoja na Mambo
mengine, mkutano huo utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya
SADC na kuweza kuona changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kupata majibu ya
kutatua changamoto hizo," Amesema Prof.
Kabudi
Makamu
wa Rais ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu
Wizara ya Ulinzi Dkt. Faraji Mnyepe pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya
Ushirikiano wa Kikanda na Mratibu Kitaifa wa Masuala ya SADC, Bibi Agnes
Kayola.
ASASI
ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la
SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu
mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.