Na Nelson Kessy, Pretoria
Ubalozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini wapewa changamoto ya kuhakikisha kuwa
unatekeleza Diplomasia ya Uchumi pamoja na Diplomasia ya Siasa iliyopo ndani ya
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM (2020-2025).
Changamoto
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge wakati alipotembelea
Ubalozi huo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujionea utendaji
kazi wa Ubalozi na mali za Serikali nchini humo.
Balozi
Ibuge ameutaka Ubalozi huo kuhakikisha kuwa unatekeleza diplomasia ya uchumi
pamoja na diplomasia ya siasa kwa weledi ili kuleta manufaa ya Taifa.
"Nawapongeza
kwa utendaji kazi wenu na nawasihi muendelee kujituma katika kazi (proactive)
katika kuwapata wawekezaji na kutengeneza kuwa ni sehemu ya mfumo wa kuleta
mabadiliko ambayo Serikali imeyapanga kupitia Ilani ya CCM ya 2020-2025,"
Amesema Balozi Ibuge.
Balozi
Ibuge pia alipongeza utendaji wa Ubalozi huo ambao pamoja na Afrika Kusini
unaiwakilisha Tanzania katika Ufalme wa Lesotho, Jamhuri ya Botswana, Jamhuri
ya Namibia na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Kadhalika Balozi
Ibuge alipokea changamoto mbalimbali zinazoikumba Ubalozi huo na Kuahidi
kuzifanyia kazi ili kuongeza tija na ufanisi wa Ubalozi.
Kwa
upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi amemueleza Balozi Ibuge mafaniko mbalimbali ya Ubalozi katika
kutekeleza diplomasia ya uchumi na siasa nchini Afrika Kusini.
Moja
kati ya mafanikio hayo ni pamoja na kuenezwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo
Serikali ya Tanzania na ya Afrika Kusini zinatarajia kusaini mkataba wa
kutumika lugha ya Kiswahili kama katika shule za Afrika Kusini mwezi wa Machi
2021.
"Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Afrika Kusini
tutasaini mkataba wa kutumika kwa lugha ya Kiswahili katika shule za Afrika
Kusini mwezi wa Machi 2021," Amesema Balozi Milanzi.
Pamoja
na mambo mengine Balozi Milanzi ameahidi kusimamia sera ya Diplomasia ya uchumi
pamoja na Diplomasia ya siasa kwa kuhakikisha kuwa ubalozi utaendelea
kuwasiliana na wawekezaji mbalimbali wa kuwekeza nchini Tanzania katika sekta
za Biashara, Madini na Mawasiliano.
Balozi
wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akiwatambulisha baadhi ya wafanyakazi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ibuge wakati alipowasili Ubalozini
leo tarehe 27 Novemba 2020
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa
Tanzania Nchini Afrika Kusini leo tarehe 27 Novemba 2020
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa watumishi (hawapo
pichani) wakati wa mkutano
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akiendesha kikao na wafanyakazi wa Ubalozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Balozi
wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akimuonesha
baadhi ya mali Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi wakati alipokuwa anakagua mali za Serikali Ubalozini
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.