Tanzania
na Pakistan zimetiliana saini mikataba miwili ya makubaliano ambayo ni mkataba
wa mashaurino ya kidiplomasia pamoja na mkataba wa kuanzisha tume ya pamoja ya
ushirikiano wa kiuchumi.
Mikataba
hiyo imesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi
wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem.
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) amesema kuwa makubaliano hayo yanatoa fursa nyingi zilizopo za
kuongeza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Pakistan hasa katika sekta ya
kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite,
pamoja na uwekezaji.
"Tanzania
na Pakistan zina uhusiano wa muda mrefu na katika mazungumzo yetu ya leo,
Balozi wa Pakistan ameeleza fursa zilizopo Pakistan ambapo fursa hizo
zikitumiwa vizuri zitanufaisha mataifa yote mawili," Amesema Prof. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri
uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Pakistan na kwamba fursa
hizo zitaendelea kuongeze ushirikiano wa diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania
na Pakistan.
Kwa
Upande wake Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem amesema kuwa
kusainiwa kwa mikataba hiyo muhimu itasaidia kukuza na kuendeleza diplomasia ya
Uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.
"Ni
imani yangu kuwa kusainiwa kwa mikataba hii miwili ya makubaliano baina ya
Serikali ya Tanzania na Pakistan kutasaidia kudumisha na kukuza uchumi kati ya
mataifa yetu," Amesema Balozi Saleem
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi akiangalia baadhi ya nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa Pakistani
nchini, Mhe. Mohammad Saleem katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem wakisaini
mikataba ya makubaliano katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.