Na mwandishi wetu
Marais
wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi waandamizi wa Serikali na
mabalozi waonaziwakilisha nchi zao hapa Nchini wamewataka watanzania kuendelea kudumisha
uzalendo, fikra na maono aliyokuwa nayo Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili
kuiwezesha Tanzania kukua kimaendeleo
Akizungumza
mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee, Rais
Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete amesema kifo cha Hayati Magufuli
hakikutarajiwa hasa wakati huu ambapo taifa lilimuhitaji na kuwasihi watanzania
kudumisha mema aliyoyaasisi kwa maslahi ya taifa.
“Kwa
kweli kifo chake hakikutarajiwa, tulitegemea kwa kweli aendelee kuliongoza
taifa kwani katika mhula wake wa kwanza aliliongoza taifa vizuri sana…….naamini
kuwa yale ambayo hayakukamilika, Rais wa Jamhuri ya Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan
atayaendeleza kikamilifu,” Amesema Dkt. Kikwete na kuwasihi watanzania kuendelea
kudumisha uzalendo, fikra na maono aliyokuwa nayo Hayati Dkt. Magufuli.
Rais
wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi nae amefika katika viwanja vya
Karimjee na kusaini kitabu cha maombolezo akifuatiwa na Aliyekuwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Gahib Bilali, Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma na pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.
Biswalo Mganga.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai nae pia amefika na
kusaini kitabu hicho akifuatiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar mhe. Zubeir Ali Maulid ambaye amesema kuwa Hayati
Magufuli katika kipindi kifupi cha uongozi wake amefanya mambo mengi
yatakayosalia kuwa historia katika taifa la Tanzania.
“Msiba
huu ni wetu sote watanzania na umetugusa sana kwani hayati Magufuli ameyafanya mengi katika mhula
wake wa kwanza ambapo mengi hayo tumekuwa tukinufaika nayo sisi watanzania…..kwa
sasa tushikamane kudumisha umoja wetu ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo,”
Amesema Mhe. Maulid
Aidha,
mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wameungana na watanzania kuomboleza
kifo cha Hayati Dkt. Magufuli kwa kusaini kitabu cha maombolezo ambapo baadhi
yao wamemuelezea kuwa katika uhai wake Hayati Magufuli alitamani kuiona
Tanzania inayojitegemea kiuchumi na watu wake kuondokana na umasikini.
Naibu
Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Mhe. Prefere Ndayishimiye amesema kuwa msiba
wa Hayati Magufuli umewagusa sana kwani alikuwa kiongozi aliyependwa na
kujulikana na bara lote la Afrika.
“Amefanya
maendeleo makubwa ambapo naamini kuwa vizazi vijavyo vitayaona na kuendeleza
pale alipoishia Dkt. Magufuli,” Amesema Naibu Balozi
Kadhalika, mbali na viongozi wastaafu pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wananchi wa kada mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kusaini kitabu cha maombolezo na kumuelezea hayati Magufuli kuwa alikuwa kiongozi aliyeweka maslahi ya nchi mbele kwa manufaa ya watanzania.
Rais wa Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021
Rais wa Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021
Makamu
wa Rais, Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo
katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma akisaini kitabu cha maombolezo katika
viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati John Pombe Joseph Magufuli
Spika
wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mhe. Zubeir Ali Maulid
akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha
aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli
Balozi
wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Ali Abdulla – Al Mahrouq akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.