Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tanzania
na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye
changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa
unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.
Ahadi
hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa
Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski leo jijini Dar es Salaam.
Prof.
kabudi amesema kuwa
Tanzania na Vatican kwa kutambua umuhimu wa amani, zimeahidi kuendelea kushirikiana
katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano
katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu duniani.
“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu
na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita……..
katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za
maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo
yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya
Demokrasia ya Kongo,” Amesema Pro. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia
inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote
duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani,
utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu
umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.
“Mfano
katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi
kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano
dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na
badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Pro.
Kabudi
Kwa
upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski
amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na
Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.
“Maongezi
yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye
maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na
masuala ya amani na usalama duniani,” Amesema Askofu Mkuu Solczynski.
Baba
Mtakatifu Papa Francisko alimteua, Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi
mpya wa Vatican nchini Tanzania mwezi Aprili, 2017. Kabla ya uteuzi huu, Askofu
mkuu Solczyński alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Georgia, Armenia na
Azerbaijan.
Katika
tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria
hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi
hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya
Tanzania na Algeria.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi,
(Mb) akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski
wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar
es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi,
(Mb) akiongea na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam
Balozi
wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski akimuelezea jambo Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb)
wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar
es Salaam
Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William
Tate Ole Nasha akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam
Balozi
wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo
ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.