Na Mwandishi wetu,
Tanzania
imejivunia mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha miaka 40 ya uanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na miaka 40 ya uanachama wa
SADC tangu 1979, lugha ya kiswahili kutumika katika mikutano yote ya kisekta ya
SADC pamoja na kutengenzwa sanamu maalumu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere.
“Pamoja
na mambo mengine, mkutano wetu wa leo wa Baraza la Mawaziri wa SADC tunategemea
kujadili masuala mbalimbali anayohusu jumuiya hiyo likiwemo suala la matumizi
ya lugha ya Kiswahili katika mikutano yote ya kisekta,” Amesema Prof. Kabudi.
Mambo
mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na suala la kutengeneza sanamu maalumu ya
Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo sanamu hiyo itawekwa
katika jengo la Amani Addis Ababa nchini Ethiopia, pamoja na maadhimisho ya
miaka 40 ya SADC.
“Hivyo
kupitia mkutano huu tutakamilisha mchakato wa kumpata mtu atakae ifua sanamu
hiyo ya Mwl. Nyerere ambapo itawekwa katika jingo la Amani Ethiopia,” Amesema
Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameendelea kueleza kuwa katika mkutano huo suala la maadhimisho ya miaka 40 ya SADC pia limejadiliwa ikiashiria umoja wa SADC kudumu kwa miaka 40.
“Miaka
40 ya SADC ina umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania kwa sababu miongoni mwa
viongozi nane walioasisi sadc ni Mwl. Julius Nyerere katika mkutano uliofanyika
mwaka 1979 mkoani Arusha ambapo Tanzania iliamua kuingia rasmi katika jumuiya
hiyo,” Ameongeza Prof. Kabudi
Tanzania
itakuwa inasherekea miaka 40 ya SADC ikiwa tayari Kiswahili ni moja ya lugha
rasmi za jumuiya hiyo, lakini pia ikiwa na sanamu maalumu ya kumuenzi na
kumheshimu baba wa Taifa na Muasisi wa SADC Mwl. Julius Nyerere.
Hivyo
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa
Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Fedha na Mipango –
Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.
Omar Said Shaaba, Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto, Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja
na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaban.
Februari
27, 2021 katika mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulifanyika
kwa njia ya Mtandao, wakuu wan chi waliridhia lugha ya Kiswahili iwe lugha ya
tatu katika shughuli za jumuiya hiyo sambamba na lugha ya kifaransa kuwa lugha
ya nne.
Kadhalika,
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika mkutano wao wa 39 uliofanyika jijini
Dar es Salaam mwezi Augusti, 2019 waliridhia na kuipitisha kiswahili nne ya
mawasiliano, ikiungana na lugha za Kifaransa, Kiingereza na Kireno zinazotumika
katika jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb), katikati pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Kaimu
Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agnes Kayola wakifuatilia mkutano
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mkutano
wa baraza la mawaziri
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (anaesoma taarifa) na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed
Mazrui (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge (kushoto) wakifuatilia
mkutano
Ujumbe
wa Tanzania ukiendelea kufuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC
Ujumbe wa Tanzania ukiendelea kufuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC Mkutano ukiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.