Wednesday, March 24, 2021

WAZIRI MKUU AONGOZA WAKAZI WA MWANZA KUMUAGA JPM

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Waombolezaji walianza kuingia uwanjani leo alfajiri na wengine wakiwa wamejipanga barabarani kuulaki msafara wa mwili wa Hayati Magufuli ukitokea Zanzibar.

Mhe. Majaliwa aliongozana na mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wa taasisi za umma na binafsi katika hafla ya kutoa heshima za mwisho kwa kwa hayati Dkt. Magufuli anayetarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Chato Machi 26, 2021.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa salamu za pole kwa wananchi wa Mwanza katika hafla kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati alipowasili katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza katika hafla kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitoa heshima za mwisho katika uwanja wa CCM Kirumba wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba    

Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa barabarani kushuhudia msafara uliobeba mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli 






 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.