Na Mwandishi wetu, Dar
Uingereza
imesema Tanzania ni mbia wake muhimu wa miaka mingi katika maendeleo na Jumuiya
ya Madola na kuahidi kuwa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya
kidiplomasia, biashara na uwekezaji.
Waziri
wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge ameyasema
hayo jijini Dar es Salaam katika mazungumzo rasmi aliyoyafanya na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula muda
mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
“Lengo
la ziara yangu hapa Tanzania ni kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya
Uingereza na Tanzania licha ya changamoto ya ugonjwa wa COVID – 19 ambapo
Uingereza tumekusudia kuisaidia Tanzania kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi, mapambano
dhidi ya rushwa lakini pia katika sekta za afya na elimu,” amesema Mhe. Duddridge.
Akizungumzia
ziara hiyo ya waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema
ziara hiyo ni kielelezo cha Tanzania kuheshimika na kukubalika miongoni mwa
Jumuiya za Kimataifa na Mataifa ya nje na kwamba kipaumbele cha Serikali ya
awamu ya sita ni diplomasia ya uchumi ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi tatu
kubwa zinazowekeza hapa nchini na hivyo kuwa ni miongoni mwa Mataifa muhimu kwa
Tanzania katika kukuza diplomasia ya uchumi.
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa katika mazungumzo yao msisitizo mkubwa umewekwa katika
uchumi na kukuza biashara pamoja na kuiendeleza miradi mikubwa iliyokuwa
ikitekelezwa na Uingereza ikiwemo miradi ya kiwanda cha sukari na madini.
“Ujio
wa Waziri wa Uingereza anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Duddridge hapa nchini inathibitisha kuwa mahusiano ya
Tanzania nje ya mipaka yake bado ni imara licha ya taarifa potofu zilizokuwa
zikisambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya nje zikitilia
mashaka juu ya diplomasia ya Tanzania nje ya nchi,” amesema Balozi Mulamula.
Aidha,
kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji Balozi Mulamula amemuhakikishia Mhe. Duddridge
kuwa mazingira ya uwekezaji ni salama na yanavutia baada ya kuboreshwa na hivyo
kumtaka kuwahamasisha wawekezaji kutoka Uingereza kuja hapa nchini kuwekeza
katika sekta mbalimbali.
Mara
baada ya mazungumzo na Balozi Mulamula Waziri Duddridge amekutana na Waziri wa
Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo pamoja na Waziri wa Uwekezaji Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe na baadae kukutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
na kesho (Jumatano) anatarajia kwenda Zanzibar kukutana na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kabla ya kuhitimisha
ziara yake ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akimkaribisha Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe.
James Duddridge katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam. Waziri
Duddridge ameambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiteta jambo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika
Mhe. James Duddridge wakati wa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za
wizara jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge akimueleza
jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula wakati wa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za
wizara jijini Dar es Salaam
Kikao
kikiendelea
Sehemu
ya wakurugenzi na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Uingereza
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge
Balozi
wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar (wa kwanza kulia) na baadhi ya
maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza wakifuatilia kikao cha Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa
Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya
Afrika Mhe. James Duddridge (mwenye tai ya bluu) pamoja na Balozi wa Uingereza
Mhe. David Concar, Maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza, Wakurugenzi kutoka
Wizarani
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.