Mkutano wa 14 Baraza la
Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa Ngazi ya Wataalam umeanza leo tarehe 21 Juni 2021 jijini Arusha ukiwashirikisha
Wataalam wa Kilimo kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Mkutano wa Wataalam utafuatiwa
na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 24 Juni 2021 na kuhitimishwa
na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 25 Juni 2021.
Lengo la Mkutano wa 14 wa
Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo
na Usalama wa Chakula pamoja na mambo mengine ni kupitia na kujadili
utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya pamoja na
kupitia na kujadili masuala mbalimbali
muhimu ya kisera, kikmkakati, miradi na program zinazotekelezwa katika
sekta ya kilimo.
Kadhalika agenda muhimu zitajadiliwa
wakati wa mkutano huo ambazo ni pamoja na Taarifa ya Usalama wa Chakula ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu Mradi wa Afrika wa Kilimo cha Ushindani
cha Mpunga kwa Kanda ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Mifugo; Taarifa
kuhusu Mradi wa Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu; Taarifa kuhusu Maendeleo ya
Uvuvi; na Taarifa kuhusu Uhamasishaji wa Uchangiaji Rasilimali.
Awali akifungua Mkutano huo
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Muthuki, Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo anayeshughilikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe.
Christophe Bazivamo amezitaka Nchi Wanachama kujikita kwenye kilimo cha
ushindani na kuboresha viwango vya mazao yanayozalishwa na nchi zote wanachama
ili kupata soko la ndani na nje ya jumuiya la mazao hayo kwa manufaa ya
wananchi wa jumuiya.
Pia amesisitiza umuhimu wa nchi
wanachama kuendelea kuwajengea uwezo wakulima katika maeneo yao kwa kutoa elimu
ya kilimo bora na chenye manufaa ili kupata mazao bora yenye viwango
vinavyokubalika ndani na nje ya mipaka ya nchi wanachama.
“Napenda kuzihimiza nchi
wanachama kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima wao pamoja na kuwajengea
uwezo ili kuwawezesha kuzalisha mazao bora na yenye viwango vinavyokubalika
ndani ya jumuiya na nje ili hatimaye wunufaike na soko la ndani na nje ya
jumuiya” alisisitiza Dkt. Muthuki kwenye hotuba yake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Mkutano huo wa Ngazi ya Wataalam, Bw. Julius Mwabu kutoka Jamhuri ya Kenya aliwataka
wajumbe wa mkutano huo kujadili na kutoa mapendekezo yenye tija kuhusu Sekta ya
Kilimo na Usalama wa Chakula kwani ni miongoni mwa sekta muhimu zinazotegemewa na
wananchi wote wa nchi wanachama wa Jumuiaya ya Afrika Mashariki.
Aliongeza kuwa, mbali na
changamoto ya ugonjwa wa corona uliozikumba nchi mbalimbali duniani zikiwemo
zile za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana
katika sekta ya kilimo na usalama wa chakula na kuwaomba wajumbe kujadili na kutoa
mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hiyo ili kuziwezesha nchi
wanachama kutotetereka katika kipindi hiki ambacho ugonjwa huo bado
haujatokomezwa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano
wa Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka
Wizara ya Kilimo, Bw. Gungu Mibavu na kuhudhuriwa pia na Maafisa Waandamizi
kutoka Sekta mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya kilimo na usalama wa
chakula hapa nchini.
|
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. Gungu Mibavu akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wataalam uliofanyika jijini Arusha tarehe 21 Juni 2021 ikiwa ni maandalizi ya awali ya Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini hapa tarehe 25 Juni 2021. Mkutano wa ngazi ya wataalam utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 24 Juni 2021. |
|
Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Bw. Julius Mwabu kutoka Kenya akiwa na Mkurugenzi wa Sekta ya Uzalishaji katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw.Jean Havugimana (kulia) pamoja na Katibu wa Mkutano huo kutoka Burundi |
|
Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Bw. Mwabu akizungumza wakati wa mkutano huo |
|
Mkurugenzi wa Sekta ya Uzalishaji kutoka Sekrtarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Havugimana naye akizungumza wakati wa mkutano wa wataalam |
|
Ujumbe wa Kenya ulioshiriki mkutano wa wataalam |
|
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Kenya ukifuatilia mkutano |
|
Mjumbe wa Burundi naye akishiriki mkutano wa wataalam |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benjamin Mwesiga akishiriki mkutano wa wataalam |
|
Ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye mkutano wa wataalam |
|
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania kutoka sekta mbalimbali zinazojishughulisha na kilimo wakifuatilia mkutano wa wataalam |
|
Mkutano ukiendelea |
|
Wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki mkutano wa wataalam |
|
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano |
|
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano |
|
Mkutano ukiendelea |
|
Mshiriki mwingine wa mkutano kutoka Tanzania |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.