Thursday, June 10, 2021

MAKATIBU WAKUU KUTOKA NCHI ZA EAC WANAOSHUGHULIKIA MIPANGO NA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA ARUSHA

Mkutano wa Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika jijini Arusha tarehe 10 Juni 2021.


Mkutano huo ambao ulitanguliwa na Mkutano kwa Ngazi ya Wataalam uliofanyika tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 jijini hapa, pamoja na mambo mengine umekamilisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika tarehe 11 Juni 2021.


Miongoni mwa agenda zitakazowasilishwa kwa Mawaziri ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kujiunga na EAC; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa ya utatu wa Jumuiya za EAC-COMESA-SADC katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika na Taarifa ya Uchangiaji wa Bajeti ya EAC kutoka Nchi Wanachama.


Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Makatibu Wakuu umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome. Viongozi wengine walioshiriki Mkutano huo ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na   Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. 

Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Dkt. Kevit Desai (kushoto) akiongoza Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021. Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili na kupitisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa Mawaziri.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome (kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Dodoma tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi

Sehemu ya ujumbe wa Kenya ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

Sehemu ya ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano wa MakatibuWakuu

Sehemu ya ujumbe wa Rwanda ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

Sehemu ya ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Sudan Kusini

Prof. Mchome akiwa amesaini Ripoti ya Makatibu Wakuu itakayowasilishwa kwa Mawaziri

Mjumbe kutoka Sudan Kusini naye akisaini Ripoti hiyo

Mjumbe wa Uganda akisaini ripoti hiyo

Mjumbe wa Kenya akisaini ripoti hiyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Mhe. Clementine Mukeka akizungumza kwa niaba ya Makatibu Wakuu wenzake walioshiriki Mkutano wa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha kwa ajili ya kuandaa  Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania

Ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.