Na Mwandishi wetu, Dar
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi
wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes kwa
lengo la kujitambulisha na kuelezea maandalizi ya ujio wa wafanyakazi wa kujitolea wa Shirika hilo kutoka Marekani.
Bibi.
Stephanie Joseph de Goes amemueleza Balozi Sokoine kuwa wafanyakazi hao
wanatarajiwa kuwasili hapa nchi kwa ajili ya kufanya kazi katika maeneo
mbalimbali yenye uhitaji.
Pamoja
na Mambo mengine, Katibu MKuu Balozi Sokoine amemhakikishia Mkurugenzi Mkazi
huyo ushirikiano na kwamba Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki
iko tayari kuratibu utendaji wa shirika hilo hapa nchini kwa kushirikiana na
Wizara nyingine za Kisekta zinazoguswa kiutendaji na Shirika hilo kwa maslahi
mapana ya pande zote mbili.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea
la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo
za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la
Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi.
Stephanie Joseph de Goes akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine Ripoti ya Mwaka ya
Shirika hilo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi.
Stephanie Joseph de Goes akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kumalizika
kwa maongezi yao
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.