Na mwandishi wetu , Lilongwe
Kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu ni miongoni mwa vikao vya awali kuelekea
Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 17 hadi 18 Agosti 2021 jijini Lilongwe,
Malawi.
Ujumbe
wa Tanzania kwenye mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu unaongozwa na
Mratibu Mkuu wa Kitaifa wa masuala ya SADC, Balozi Agnes Kayola ambaye
amemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Joseph Sokoine.
Viongozi
wengine walioambatana na Balozi Kayola
kwenye mkutano huo ni pamoja na: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,
Bi. Amina Shaaban ambaye ameongoza Kikao cha Kamati ya Fedha katika kikao hicho
cha Makatibu Wakuu; na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.
Aidha,
mkutano huu utafuatiwa na mikutano mingine ya awali ikiwamo Mkutano wa Baraza
la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafanyika tarehe
13 hadi 14 Agosti, 2021 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya
Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC utakaofanyika tarehe 16 Agosti
2021 ambao utajadili hali ya ulinzi na usalama katika kanda kwa kipindi cha
Agosti 2020 hadi Agosti 2021. Mkutano huu utahusisha nchi tatu (3) za SADC Organ
Troika ambazo wajumbe wake ni Botswana, Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya
Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Afrika Kusini, Mwenyekiti ajaye wa
Organ; na Zimbabwe, Mjumbe aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi.
Ujumbe
wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utaongozwa na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ambaye ataambatana na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwakilishi kutoka
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mikutano
hii ya awali pamoja na mambo mengine inajukumu la kuandaa, kupitia na kuwasilisha
mapendekezo ya masuala mbalimbali ya kikanda yatakayofanyiwa maamuzi kwenye
Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika utakaofanyika tarehe 17-18 Agosti 2021 jijini Lilongwe.
Mkutano
wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu ulianza tarehe 9 Agosti 2021 na
unatarajiwa kumalizika leo tarehe 11 Agosti 2021. Kumalizika kwa mkutano huu
kunaruhusu kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.