Balozi Fatma Rajab akizungumza katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam |
Balozi Fatma Rajab
(kushoto) akizungumza katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es
Salaam
Balozi Fatma Rajab
(katikati) akiwa meza kuu wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es
Salaam
Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es
Salaam wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mkutano huo
Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es
Salaam wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Fatma Rajab amefunga Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa Utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo pia uliangalia changamoto ambazo nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unakabiliana nazo katika kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo na kuzitafutia njia ya kukabiliana nazo pamoja na matarajio ya kuanzishwa kwa Mahakama hiyo.
Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huo Balozi Fatma amewataka washiriki wa mkutano huo kuyachukua yale yote waliyokubaliana katika mkutano huo ili kuziwezesha nchi zao kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo kwa ufanisi.
Mkutano huo ulianza Novemba Mosi umehudhuriwa na Wanasheria waandamizi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.