Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshiwa Yoweri Kaguta Museveni wakikata utepe wakati wakuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi ya "Museveni Pre & Primary School" iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita
******** Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda leo tarehe 29 Novemba, 2021 amehitimisha ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini, na kurejea nchini Uganda ambapo ameagwa rasmi na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Geita uliopo wilayani Chato.
Akiwa Wilayani Chato, Rais Museveni amekabidhi majengo ya Shule ya Awali na Msingi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyopo katika kijiji cha Nyabilezi wilayani Chato. Ujenzi wa Shule hiyo umegharimu jumla ya Dola za Marekani Milioni 1.67, yamefanyika wakati muafaka ambapo itaongeza fursa kwa wanafunzi wote kupata elimu hata kwa wale wenye mahitaji maalum.
Rais Samia sambamba na kupokea majengo ya shule hiyo ameelezea kuwa shule hiyo ni matunda ya ushirikiano na uhusiano mzuri uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Uganda. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.