Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka
107 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 76 tangu kumalizika
kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya
Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (katikati) pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar na baadhi ya Mabalozi kutika nchi za Jumuiya ya Madola wakifuatilia kumbukizi ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 107 tangu
kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 76 tangu kumalizika kwa vita ya
pili ya dunia
Viongozi na wananchi wakifuatilia kumbukizi ya
maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 107 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya
dunia na miaka 76 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini, Mhe. David Concar pamoja na Balozi wa Ujerumani Nchini, Mhe. Regina Hess wakienda kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Canada Nchini, Mhe. Pamela O’Donnel pamoja na Balozi wa Pakistan Nchini,
Mhe. Muhammad Saleem wakienda kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu
wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia katika makaburi ya
Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Marekani Nchini, Mhe. Donald Wright pamoja na baadhi viongozi wakitoa
heshima mara baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa
mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia katika makaburi ya
Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, Balozi
wa Uingereza Nchini, Mhe. David Concar pamoja na Balozi wa Ujerumani Nchini,
Mhe. Regina Hess wakiweka shada la maua katika mnara wa askari ulioko Posta
Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 107 tangu
kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 76 tangu kumalizika kwa vita ya
pili ya dunia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 107 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 76 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.