Na Mwandishi wetu, Roma
Shirika
la Taifa la Madini (STAMICO) limesaini mkataba wa makubaliano ya awali na
Kampuni ya Suness Limited ya Italia kwa ajili ya kuendeleza mradi mkubwa wa Shaba
katika Mkoa Kilimanjaro. Suness Limited ni kampuni ya Kiitaliano
inayojishughulisha na uchimbaji madini na Kampuni hiyo imeonesha utayari wa
kushirikiana na STAMICO katika kuendeleza kwa pamoja mradi wa shaba.
Akiongea
mara baada ya kusaini mkataba huo leo Jijini Roma Italia, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance
Mwasse amesema kuwa mkataba umesainiwa kupitia jukwaa la biashara na uwekezaji
lililofanyika Jijini Roma Italia tarehe 02 – 03 Disemba 2021.
Pamoja
na mambo mengine, STAMICO wameweza kuelezea juu ya mradi wa mkubwa wa shaba
unaopatikana katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo pia mwekezaji ameonesha nia ya kuingia ubia na STAMICO.
“Shirika
lina mradi wake mkubwa wa Shaba mkoani Kilimanjaro wenye kiasi kikubwa cha
mashapu ya Shaba na kupitia jukwa la wafanyabiashara na uwekezaji lililofanyika
Roma Italia, tumewaeleza juu ya mradi huo na wenzetu wameonesha kuvutiwa na
mradi huo na tukakubaliana kusaini makubaliano ya awali na baadae watakuja Tanzania
ili kwa pamoja twende kwenye eneo la mradi husika na mwishowe tuingie katika
makubaliano ya pamoja ya kuendeleza mradi huo,” Amesema Dkt. Mwasse
Naye
Rais wa Kampuni ya Sunless Bw. Sandro Calo amesema kuwa amefurahishwa na utiaji
saini wa awali wa mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kushirikiana na Serikali
ya Tanzania katika kuendeleza kwa pamoja mradi wa Shaba
“Nimefurahia
kuanza kwa makubaliano haya mapya ambayo yataleja matokeo chanya kati ya nchi
ya Tanzania na Italia na naahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa maslahi mapana
ya pande zote mbili katika sekta hii ya madini,” amesema Bw. Calo.
Utiaji
saini wa makubaliano hayo umeshuhudiwa
na Naibu Waziri, Wizara ya Madini Mhe. Prof. Shukrani Manya, Balozi wa
Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo, Mkurugenzi Idara ya
Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya
Zanzibar Classic Safaris, Bw. Yussuf Salim Njama.
Mkurugenzi
Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse pamoja na Rais wa Kampuni ya Sunless
Bw. Sandro Calo wakisaini mkataba wa makubaliano ya awali kwa ajili ya
kuendeleza mradi mkubwa wa Shaba katika Mkoa Kilimanjaro. Utiaji saini wa
mkataba huo umeshuhudiwa na Naibu
Waziri, Wizara ya Madini Mhe. Prof. Shukrani Manya, Balozi wa Tanzania Nchini
Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo pamoja Mkurugenzi Idara ya Diplomasia ya Uchumi
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin
Rutageruka Jijini Roma, Italia.
Mkurugenzi
Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse akibadilishana mkataba wa makubaliano
ya awali kwa ajili ya kuendeleza mradi mkubwa wa Shaba katika Mkoa Kilimanjaro na
Rais wa Kampuni ya Sunless Bw. Sandro Calo mara baada ya kusainiwa wakisaini kwa
mkataba huo leo Jijini Roma, Italia
Mkurugenzi
Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse pamoja na Rais wa Kampuni ya Sunless
Bw. Sandro Calo wakionesha mkataba wa makubaliano ya awali kwa ajili ya
kuendeleza mradi mkubwa wa Shaba katika Mkoa Kilimanjaro na mara baada ya
kusainiwa leo Jijini Roma, Italia
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.