Na Mwandishi wetu, Roma
Wawekezaji
zaidi ya 140 kutoka Italia wamewekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania
Takwimu
hizo zimetolewa na Naibu Waziri Wizara ya Madini, Prof. Shukrani Manya alipokuwa
akifungua jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika
leo Jijini Roma, Italia.
Prof.
Manya amasema kuwa miradi hiyo inathamani ya Shilingi bilioni 5 inayotoa ajira
kwa watanzania zaidi ya 4000.
“Jukwa
hili tunataka liendelee kuwa sababu ya kuchagiza uwekezaji mwingine kutoka
Italia kwa kutumia teknolojia waliyonayo, kwa kutumia utalaamu walionao wa 'designing'…….na sasa waone kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza na
Tanzania inaendelea kuweka mazingia wezeshe ya kukuza sekta ya uwekezaji na
biashara,” Amesema Prof. Manya
Ameongeza
kuwa kupitia jukwaa la biashara na uwekezaji biashara na uwekezaji utaendelea
kuongezeka na kuongeza zaidi na hasa katika maeneo ambayo tumawaeleza hapa
kupitia jukwaa hili.
Kwa
upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo
amesema kuwa kufanyika kwa kongamano hili la biashara na uwekezaji lengo lake
kubwa ni kuwavutia wafanyabiashara na wewekezaji wa sekta mbalimbali kutoka
Italia kuwekeza zaidi Tanzania.
“mwitukio
ni mkubwa na tumeitikiwa na jumuiya za kibiashara na wafanyabiashara na
wawekezaji zaidi ya 250 kutoka nchi zote mbili wameshiriki katika kongamano
hili,” amesema Balozi Kombo
Balozi
Kombo ameongeza kuwa, Wafanyabiashara kutoka italia ni wabobezi katika sekta ya
madini lakini pia katika utalii hivyo ni matumanini yake kuwa mara baada ya
kumalizika kwa kongamano hilo wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Italia
wataongezeka zaidi Tanzania.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Chama Wawekezaji katika Hoteli Zanzibar, Bw. Paulo
Rosso amewasihi wawekezaji kutoka Italia kuwekeza kwa wingi Tanzania kwa kuwa
mazingira ya biashara na uwekezaji ni tulivu na salama.
“Tanzania
ni sehemu salama kuwekeza…..nawahakikishia mimi nimewekeza Tanzania na ninaona
ni sehemu salama ya kuwekeza karibuni sana kuwekeza kwa maendeleo ya Tanzania
na Italia,” amesema Bw. Rosso
Aidha,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amewahakikishia
wafanyabiashara na wawekezaji walioshiriki katika jukwaa hilo kuwa CRDB ipo
tayari kutoa mikopo kwa watakao kuwa tayari kuwekeza Tanzania.
“Nawahakikishia
kuwa Benki ya CRDB itawawezesha mikopo ya kuwekeza katika sekta mbalimbali
hivyo msiwe na wasiwasi kuhusu mitaji ya kuwekeza ipo karibuni sana tuijenge
Tanzania,” Amesema Bw. Nsekela.
Jukwa hilo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limehudhuriwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji takribani 250 kutoka nchi zote mbili. Wafanyabiashara na wawekezaji hao ni wa sekta za utalii, kilimo, madini, na ujenzi.
Pamoja
na mambo mengine, jukwaa hilo limewawezesha wafanyabiashara na wawekezaji
kujadili fursa, uwezekano wa ubia, changamoto zinazokabili mazingira ya
biashara na njia ya kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kushirikiana na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Taifa ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
Naibu
Waziri, Wizara ya Madini Prof. Shukrani Manya akihutubia Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika leo Jijini Roma
Naibu
Waziri, Wizara ya Madini Prof. Shukrani Manya akihutubia wafanyabiashara na wawekezaji walioshiriki katika Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika leo Jijini Roma
Balozi
wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo akiongea na
wafanyabiashara waliojitokeza kushiriki Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na Italia lililofanyika leo Jijini Roma
Balozi
wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo akiongea na
wafanyabiashara waliojitokeza kushiriki Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na Italia lililofanyika leo Jijini Roma
Mkurugenzi
wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka akitoa hotuba yake kwa wafanyabiashara (hawapo pichani) walioshiriki Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika
Jijini Roma
Mwenyekiti
wa Chama Wawekezaji katika Sekta ya Hoteli Zanzibar, Bw. Paulo Rosso akiongea
na Wafanyabiashara na Wawekezaji walishiriki katika Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika Jijini Roma
Mmoja
wa Wafanyabiashara kutoka Italia akiongea na Wafanyabiashara na Wawekezaji
walishiriki katika Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia
lililofanyika Jijini Roma
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akitoa hotuba yake kwa wafanyabiashara na
Wawekezaji walishiriki katika Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania
na Italia lililofanyika Jijini Roma
Sehemu
ya Wafanyabiashara na Wawekezaji walishiriki katika Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika Jijini Roma
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.