Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)
amefanya mkutano kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann
Linde katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Viongozi
hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati
ya Tanzania na Sweden ikiwemo vipaumbele vya pande zote mbili kuelekea Mkutano
wa Wakuu wa Nchi baina ya nchi za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika (European
Union - African Union Summit) uliopangwa kufanyika tarehe 17 – 18 Februari
2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan yakiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.