Mkutano wa Makatibu Wakuu ulitanguliwa na mkutano wa Maafisa Waandamizi
uliofanyika tarehe 8 na 9 Februari 2922. Hii ni mikutano ya awali
kwaajili ya maandalizi ya Mkutano wa 15 Wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika kesho tarehe 11 Februari 2022.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu umeongozwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Tanzania Bara), Mhandisi Felchesmi Mramba ambaye ameambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Zanzibar, Dkt. Mngereza Miraji.
Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Makatibu Wakuu umepitia
na kuandaa: Taarifa ya hali ya utekelezaji wa maagizo ya mikutano
iliyopita; Hatua iliyofikiwa hadi sasa katika sekta za Nishati Umeme, Nishati
Mafuta, na Nishati Jadidifu; pamoja na Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa
na Kikanda ya Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano mwenyekiti wa mkutano huo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wa Jamhuri ya
Kenya, Maj. Gen. Dkt. Gordon Kihalangwa, CBS alieleza kuwa uhaba wa nishati
ndani ya nchi zetu na jumuiya kwa ujumla huleta changamoto kwa wananchi wote na
kushusha shughuli za uchumi na pato la taifa kwa ujumla. Hivyo, akasisitiza
umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kutekeleza miradi ya nishati ya kitaifa na
kikanda.
Vilevile akaeleza umuhimu wa sekta ya afya
kupatiwa nishati ya kutosha na ya uhakika ili kuondoa changamoto za mara kwa
mara zinazochangia kukosekana kwa huduma hizo.
“Huduma za mama na mtoto pamoja na
huduma nyingine za afya ni muhimu zikazingatia upatikanaji wa nishati ili
kupunguza matatizo yatokanayo na kukosekana kwa nishati ya uhakika kwa baadhi
ya vifaa vinavyohitaji nishati ya umeme na gesi” alisema Dkt. Gordon.
Mkutano huu umefanyika kwa njia ya mseto
ambapo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda wameshiriki mkutano wa ana kwa ana
isipokuwa Burundi, Rwanda na Sudan Kusini wameshiriki kwa njia ya mtandao.
Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia majadiliano katika mkutano huo. |
Ujumbe wa Tanzania |
Mkutano ukiendelea |
Ujumbe kutoka Uganda |
Ujumbe kutoka Kenya |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.