Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amesema Wizara kwa kushirikiana na Wizara zingine, Mashirika na Taasisi za Serikali na Sekta binafsi itaendelea kuweka jitihada katika kutangaza fursa za uwekezaji zinazotokana na sekta ya nishati.
Waziri Mulamula ameeleza haya wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ocean Business Partners Tanzania Ltd Bw. Abdulsamad Abdulrahim na Makamu wa Rais, wa Kampuni ya dmg event ya nchini Uingereza Bw. Damian Howard yaliyofanyika Ofisini kwake jijini Dodoma. “Licha ya hazina kubwa tuliyonayo katika sekta ya nishati, serikali pamoja sekta binafsi bado tunakazi kubwa ya kuendelea kutangaza na kutafuta wawekezaji ili kukuza uwekezaji na mapato katika sekta hii. Waziri Mulamula.
Bwana Abdulsamad na Bw. Howard wamepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi madhubuti wa Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. Waliongeza kusema Makampuni yao yataendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutangaza fursa za uwekezaji zinazotokana na sekta ya nishati nje ya mipaka ya Tanzania.
Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Mazungumzo yakiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.