Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula (Mb) amewasilisha kwa njia ya mtandao salamu za pongezi ya
Miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi Wanachama wa Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian
Ocean Rim Assocaition-IORA) yaliyofanyika jijini Mapou, Mauritius tarehe 7
Machi 2022. Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imewakilishwa
na Balozi Agnes Richard Kayola, Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda
aliyeambatana na Dkt. Mnata Resani, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya
Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Katika Maadhimisho hayo, nchi wanachama zimepata fursa ya kutangaza Utamaduni wao kwa kupitia vyakula, nyimbo na ngoma za asili. Tanzania iliandaa chai na kahawa ya hapa nchini na Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) kilitumbwiza kwenye maadhimisho hayo. |
Watu mbalimbali wakichukua vyakula vya Kitanzania vilivyoandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi Wanachama wa Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Assocaition-IORA) yaliyofanyika jijini Mapou, Mauritius tarehe 7 Machi 2022. |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Mhe. Alan Ganoo |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.