Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Mabalozi Wastaafu nchni na baadhi ya viongozi wa Wizara wakati wa hafla ya kukabiddhiwa Ofisi kwa Chama hicho zilizofanyika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umekabidhi ofisi kwa chama cha mabalozi Wastaafu nchini (ARTA).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekabidhi ofisi hizo zilizopo katika jengo la Wizara jijini Dar es salaam kwa niaba ya Wizara na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa wizara na watumishi .
Akikabidhi ofisi hizo Balozi Mulamula amesema ofisi hiyo iliyoko katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam itatatumiwa na mabalozi wastaafu hapa nchini ili kuwawezesha mabalozi hao kuendelea kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa hususani katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Akizungumza kwa niaba ya chama cha mabalozi wastaafu Mwenyekiti wa chama hicho Balozi Celestine Liundi amesema chama hicho kwa sasa kina wanachama hai 57 ambao bado wanaweza kuisaidia nchi katika nyanja ya uhusiano wa kimataifa.
Balozi Liundi ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kitendo cha kuwapatia ofisi ndani ya jengo la Wizara na kuongeza kuwa kitendo hicho kimewatia moyo wa kuendelea kutoa ushauri,mapendekezo na michango ya mawazo katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Mataifa mengine.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.