Nchi za Tanzania na Morocco zimeanza kuangazia namna ya kushirikiana katika masuala ya Diaspora. Haya yamejiri kwenye mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 13 Aprili 2022 baina ya Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tagie Daisy Mwakawago na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mheshimiwa Zakaria El Guomiri katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika hatua ya awali ya kuanzisha ushirikiano huo wamegusia kuanzisha jukwaa la pamoja litakalowakutanisha pamoja Diaspora wa Tanzania na Morocco ili waweze kubadilishana uzoefu, ujuzi na kunufaika na fursa zinazopatikana katika nchi zote mbili.
Bi. Mwakawago katika mazungumzo hayo amebainisha kuwa amevutiwa na hatua iliyofikiwa na Ufalme wa Morocco katika kushughulikia masuala ya Diaspora. “Nimevutiwa sana na namna mnavyofanya vizuri kwenye kushirikisha Diaspora wenu katika kuchangia pato la nchi. Natambua kuwa Daispora wenu wanachangia takribani asilimia 6 ya jumla ya pato la nchi ni hatua nzuri sana, bila shaka tukishirikiana vyema katika eneo hili itakuwa ni fursa nzuri kwetu kuendelea kujifunza na hatimaye nchi zetu zitanufaika zaidi kutokana na kuongezeka kwa uwigo wa fursa miongoni mwa Diaspora wetu” Alisema Bi. Tagie Daisy.
Kwa upande wake Balozi wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Guomiri, amepongeza jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Diaspora. Ameongeza kuwa jitihada hizo ndizo zilizomsukuma kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Tagie Daisy ili aweze kutoa uzoefu na mchango wa mawazo ambao utasaisaidia zaidi Serikali kunufanika na mchango wa Diaspora katika kuendeleza uchumi wa nchi. “Morocco tumefanikiwa kutumia programu mbalimbali ambazo zimetusaidia kutuweka karibu na kuwaunganisha Diaspora wetu wapatao milioni 6 waliopo sehemu mbalimbali duniani. Hutua hii imetusaidia kuendelea kunufaika na mchango wao katika kukuza uchumi wa Nchi. Nimefurahi kupata fursa ya kuongea na Kaimu Mkurugenzi Bi. Tagie Daisy ambapo tumepata fursa ya kuangalia namna mbalimbali ya kushirikiana katika eneo hili” Amesema Balozi Guomiri.
Ushirikiano baina Tanzania na Morocco katika masuala ya Diaspora na kuanzishwa kwa jukwaa la kuwaleta pamoja Diaspora wa pande hizi mbili kuchochea ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini.
Mazungumzo yakiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.