BALOZI NJALIKAI AKUTANA NA BALOZI WA KWANZA WA ALGERIA NCHINI TANZANIA
Balozi
wa Tanzania Nchini Algeria Mhe. Iman Njalikai amekutana na kuzungumza
na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Marafiki wa Algeria tangu kipindi cha
Ukombozi ambaye alikuwa Balozi wa Kwanza wa Algeria nchini Tanzania
Mhe. Noureddine DJoudi .
Mazungumzo na Balozi huyo mwenye
historia na kumbukumbu kubwa ya uhusiano wa Algeria na Tanzania
yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers.
Mheshimiwa
Balozi Joudi alifika Ubalozini kufuatia mwaliko wa Balozi Njalikai kwa
lengo la kufahamiana na kumpongeza kwa majukumu mapya aliyokabidhiwa na
Serikali ya Algeria.
Katika mazungumzo yao Balozi Njalikai
alimshukuru Balozi Joudi kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika
kuimarisha uhusiano kati ya Ubalozi na Mamlaka mbalimbali za Algeria
ikiwemo sekta binafsi.
Mhe. Balozi Joudi ameuomba Ubalozi kuimarisha
kituo cha Kiswahili kilichopo Ubalozini hapo kwa lengo la kuitangaza
Lugha hiyo na kuifundisha kwa Wa' Algeria wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.