|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan aliyefika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb)
akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan
aliyefika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada
ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. |
|
Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan
akizungumza na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada
ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb)
na ujumbe wake (kulia) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan
na ujumbe wake (kushoto) walikutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika picha na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan
alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada
ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akimkabidhi zawadi ya picha ya Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan
alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada
ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.), ameagana na Balozi wa India anayemaliza muda wake wa uwakilishi nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam tarehe 10 Januari, 2024, Mhe. Waziri Makamba amemshukuru Mhe. Binaya kwa jitihada zake za kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na India unakua na kuimarika.
Amempongeza pia kwa mafanikio yaliyopatikana kupitia ziara iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India na kufanikisha kusainiwa kwa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano wakati wa ziara hiyo.
Naye Mhe. Balozi Binaya ameshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla wakati wote wa kipindi chake alichohudumu nchini.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.