 |
| Naibu
Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore (kulia) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata wakizindua kitabu
kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha
ya Kiswahili katika hafla iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 01 Machi 2024. |
 |
| Naibu
Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu
kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa
lugha
ya Kiswahili |
 |
| Mkurugenzi wa
Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Resani
Mnata akimkabidhi nakala ya kitabu mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Naomi Zegezege katika hafla ya kuzindua kitabu
kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa
lugha
ya Kiswahili |
 |
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta (katikati) aliposhiriki hafla ya uzinduzi wa kitabu
kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa
lugha
ya Kiswahili iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro
|
 |
| Naibu
Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa kitabu
kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa
lugha
ya Kiswahili |
 |
| Naibu
Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa
Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Resani
Mnata , Balozi wa Tanzania Ujerumani (wa pili kulia) wakitoa heshima katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati wa utawala wao |
 |
| Naibu
Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiweka shada la maua katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati
wa utawala wao |
 |
| wananchi wa kabila la Kichaga wakicheza ngoma za asili wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa
lugha
ya Kiswahili |
Naibu
Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul ameshiriki uzinduzi wa kitabu
kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la kichaga kilichoandikwa kwa lugha
ya Kiswahili.
Wakati
wa uzinduzi ambao umefanyika katika kigango cha Kidia, Old Moshi, imeelezwa kuwa kitabu hicho
ambacho kimetafsiri kazi ya mwandishi mchungaji Bruno Gutmann, kinalenga
kutambua utumishi wa mchungaji huyo raia wa Ujerumani ambaye aliishi eneo hilo
kwa miaka 28 na kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo huku akieneza injili.
Kitabu
hicho ni miongoni mwa vitabu 400 vilivyoandikwa kwa lugha ya Kijerumani na
mchungaji huyo ambapo mpaka sasa vitabu vitano vimeandikwa kwa lugha nyingine ikiwemo kichaga na kiswahili.
Uzinduzi
huo pia umeshuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kısare Makore, Balozi wa Tanzania nchini
Ujerumani, Mhe. Hassan Mwamweta na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata.
Naibu
Waziri Keul yuko nchini kwa ziara ya siku nne ya kikazi kuanzia tarehe 29
Februari hadi Machi 4 2024.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.