Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akifuatilia mkutano |
Mkutano ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akifuatilia mkutano |
Mkutano ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea jijini Dodoma na kuhitimishwa leo tarehe Mei 31, 2024.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao huku ujumbe wa Tanzania ukishiriki kutokea jijini Dodoma, Balozi Mussa amesema zipo fursa nyingi katika Jumuiya hiyo ambazo Tanzania ikijipanga itanufaika nazo ikiwemo utunzaji wa mazingira na rasilimali za bahari, ulinzi na usalama baharini, namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uvuvi na utalii na kwamba wakati umefika sasa wa kuhakikisha wananchi wa Tanzania wananufaika kupitia jumuiya hiyo.
Aidha, kupitia mkutano huo Balozi Mussa amewasisitiza wajumbe wa mkutano waliotoka katika Taasisi, Wizara na Idara za Serikali kuendelea kuhakikisha maazimio mbalimbali yanayofikiwa kupitia Jumuiya hiyo yanatekelezwa kikamilifu ili kulinufaisha taifa kiuchumi na kijamii kwa ujumla.
“Ninawahimiza tuendelee kushirikiana ili taarifa za utekelezaji wa maazimio ya mkutano huu yaweze kufanyiwa kazi kwa haraka na kuiwezesha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kuratibu shughuli za kikanda na kimataifa kwa tija na maslahi mapana ya Nchi’’ alisema Balozi Mussa.
Kadhalika wakati wa Mkutano huo, Tanzania iliwasilisha pendekezo la Mradi kuhusu Ushirikishwaji wa Jamii za Pwani katika Utunzaji wa Rasilimali za Bahari za ukanda wa Pwani ambalo linalenga pamoja na mambo mengine kuzijengea uwezo jamii za Pwani kutunza rasilimali za bahari na kuibua fursa za kiuchumi zitakazowanufaisha na kuinua kipato cha wananchi wa ukanda wa Pwani.
Akiwasilisha pendekezo hilo, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Saida Fundi amesema Chuo hicho kilikuja na wazo la kuandaa mradi huo baada ya kuona upo umuhimu mkubwa wa kuziwezesha jamii zilizopo kwenye mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi kunufaika na rasilimali zitokanazo na bahari.
Amesema pendekezo la mradi huo ambalo litahusisha Warsha itakayofanyika hapa nchini mwezi Oktoba 2024 na kuzihusisha nchi wanachama na wadau mbalimbali lina malengo mahsusi ikiwemo kuimarisha mtandao wa watumiaji wa rasilimali za bahari katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi na kuzijengea uwezo jamii za ukanda wa Pwani ili kunufaika na fursa mbalimbali.
========================
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano. |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. |
Mkutano ukiendelea. |
Katibu Mkuu, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi akizungumza |
Washiriki wa jukwaa hilo wakifuatilia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024 |
Washiriki wa jukwaa hilo wakifuatilia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024 |
Washiriki wa jukwaa hilo wakifuatilia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024 |
Washiriki wa jukwaa hilo wakifuatilia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024 |
Washiriki wa jukwaa hilo wakifuatilia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024 |
Washiriki wa jukwaa hilo wakifuatilia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024 |
meza kuu katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa jukwaa hilo |
Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umeratibu na kushiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia lililofanyika jijini Windhoek tarehe 30 Mei 2024.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi,ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Jukwaa hilo.
Jukwaa hilo limejumuisha Sekta za Kilimo, Mifugo, Utalii, Biashara na Uwekezaji.
Picha ya pamoja |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka akifuatilia Mkutano |
Ujumbe wa Tanzania ukifatilia mkutano. |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ikifuatilia mkutano. |
Picha ya pamoja. |
Mkutano ukiendelea. |
Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe maji katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Amos Madalla akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Kawaida wa Sita wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uvuvi na Ukuzaji Viumbe maji katika Ziwa Victoria la EAC kwa Ngazi ya Wataalam unaoendelea jijini Arusha |
Mkutano ukiendelea |
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Dorah Neema akichangia jambo kwenye Mkutano wa Kawaida wa Sita wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uvuvi na Ukuzaji Viumbe maji katika Ziwa Victoria la EAC kwa Ngazi ya Wataalam unaoendelea jijini Arusha |
Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji na Masuala ya Jamii Bw. Aime Nkurunziza na mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uvuvi na Ukuzaji Viumbe maji EAC akiongoza mkutano wa Baraza hilo katika ngazi ya Wataalamu uliofanyika jijini Arusha |
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeridhia na kupitisha makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Shillingi Bilioni 241 kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Jijini Dodoma leo Mei 28, 2024
Awali akiwasilisha bungeni hotuba yake, Waziri Mhe. January Makamba amelieleza Bunge kuwa katika mwaka ujao wa fedha, Wizara imejipanga kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa nguvu mpya ili kuchochea Uwekezaji, Utalii, na Biashara pamoja na kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa maendeleo ya Nchi.
Kadhalika amesema, Wizara itaendelea kukuza ushirikiano wa uwili wa kimkakati pamoja na kuhakikisha ushiriki wenye tija wa Tanzania katika jumuiya na mashirika ya kikanda na kimataifa ili kulinda maslahi mapana ya taifa; pamoja na kustawisha diplomasia ya kisasa na kujenga uhusiano wa karibu na nchi washirika.
Amesema kipaumbele kingine kwa Wizara ni kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi, kuimarisha utawala bora na rasilimaliwatu pamoja na kutekeleza miradi ya ujenzi, ununuzi na ukarabati wa majengo ya ofisi, makazi ya watumishi na vitega uchumi katika Balozi za Tanzania na makao makuu.
Mhe. Makamba amelifahamisha Bunge kuwa, Wizara imekamilisha rasimu ya awali ya Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ambao umeainisha maeneo saba ya kipaumbele ambayo Wizara itayatilia mkazo katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ikiwemo Kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje; na Kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi.
Maeneo mengine ni kuvutia watalii kuja Tanzania; Kutafuta misaada na mikopo ya masharti nafuu kutoka nje; Kutafuta fursa za ajira na masomo kwa Watanzania nje ya nchi; Kujenga taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa na Kujenga uwezo wa kitaasisi wa Wizara, na Wizara na Taasisi nyingine kusimamia vizuri utekelezaji wa Mkakati wa Diplomasia ya Uchumi.
Kuhusu Diaspora, Mhe. Makamba amesema Wizara inatambua mchango wao katika maendeleo ya nchi na kwamba Serikali imejumuisha masuala ya Diaspora katika mapitio ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 na Sera Mpya ya Ardhi ya 2024 na kutoa Hadhi Maalum (Special Status) kwa Raia wa Nchi Nyingine Wenye Asili ya Tanzania ili kuwapa haki na upendeleo mahsusi.
Amesema katika kutekeleza jukumu hilo, mwezi ujao, Serikali itawasilisha katika Bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria utakaokuwa na marekebisho madogo ya Sheria za Uhamiaji Sura ya 54 na Sheria ya Ardhi Sura ya 113 nia ikiwa ni kukamilisha utoaji wa Hadhi Maalum kwa Raia wa Nchi Nyingine Wenye Asili ya Tanzania.
Katika medani za kimataifa na kikanda Mhe. Makamba amelijulisha Bunge kuwa, sauti ya Tanzania imeendelea kusikika na kukubalika ambapo kuanzia mwezi Agosti, 2024 Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), nafasi ambayo itaiwezesha Tanzania kuratibu na kuongoza majadiliano na maamuzi yote yanayohusu masuala ya siasa, ulinzi na usalama.
Aidha, nafasi hii itaimarisha ushawishi wake katika ukanda wa SADC katika masuala haya hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Waasisi wa SADC walioshiriki kwa hali na mali katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.
Aidha, Mhe. Makamba ametumia jukwaa hilo kuwahimiza watanzania wenye sifa, wakiwemo Wabunge kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika taasisi za kikanda na kimataifa huku akimpongeza Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile (Mb.) kwa kujitokeza kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani – Kanda ya Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Bajeti hiyo ya Wizara ambayo imeainisha vipaumbele mbalimbali imewasilishwa tarehe 28 Mei 2024 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza wakati Wizara ilipowasilisha Bungeni jijini Dodoma Hotuba ya Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato akizungumza wakati Wizara ilipowasilisha Bungeni jijini Dodoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 |
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharik, Balozi Said Shaib Mussa wakati wa uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma |
Viongozi wa Wizara wakifuatilia Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ikiwasilishwa. Kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa anayeshughulikia Siasa, na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdallah Hamid |
Mkuu wa Itifaki, Balozi Yusuph Mndolwa (kushoto) akiwa Bungeni na wageni wengine waalikwa walioshiriki uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma |
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim akiwa Bungeni kwa ajili ya kushiriki uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirikia waliopo nchini wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara |