Kikao kikiendelea
kikao kikiendelea |
Kikao kikiendelea |
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda amekutana na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Djibouti Balozi Guelleh Idriss Omar katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi Guelleh Idriss Omar yuko nchini na Ofisi ya Uratibu wa Kitaifa ya Djibouti kuhusu Uhamiaji (BCNM) kwa ziara ya kubadilishana uzoefu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu masuala ya uhamiaji kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM)
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uwezo wa wawakilishi wa Serikali ya Djibouti katika usimamizi wa uhamiaji, kubadilishana na wadau muhimu kuhusu mbinu bora za usimamizi wa uhamiaji, kuendeleza ushirikiano kati ya nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania, na kubadilishana uzoefu wa kivitendo katika usimamizi wa uhamiaji kati ya Djibouti na mamlaka za Tanzania.
Katika kikao hicho Balozi Kaganda aliithibitishia Djibouti dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kudumisha uhusiano wa karibu wa kikazi na Serikali ya Djibouti, kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano na ubia kati yan chi hizo mbili.
Naye Balozi Guelleh Idriss Omar ameshukuru nafasi ya kujifunza juu ya namna Tanzania inavyooendesha shughuli za uhamiaji wa kimataifa na uhusiano na nchi nyingine na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili.
Wajumbe
wengine katika ziara hiyo ni pamoja na Bi. Ifrah Ali Ahmed, Mshauri Mkuu wa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Mohamed Houmed Abasse, Mkuu wa Wilaya ya
Tadjourah, Bw. Hassan Abdi Robleh, Mkuu wa Mkoa wa Dikhil, Bi. Amana Awaleh
Oumar, anayehusika na ulinzi katika BCNM, Bi. Hasna Omara Farah, anayehusika na
maendeleo katika BCNM, na Bw. Abdallah Mohamed Bourhan, Afisa Mradi wa Kitaifa
(BMM) - IOM Djibouti.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.