Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe.Said Yakubu akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Gilead Teri alipowasilia katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam. |
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe.Said Yakubu (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Gilead Teri (kulia) katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe.Said Yakubu amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Gilead Teri katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hay, Mhe. Balozi na Bw. Teri wamejadili namna ya kukuza uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro ambako Balozi huyo anaenda kuiwakilisha Tanzania.
Kupitia mazungumzo hayo TIC imeahidi kupeleka ujumbe wa kwanza wa wawekezaji angalau 20 mwishoni mwa mwezi Juni 2024 na itashirikiana na Taasisi za sekta binafsi kuandaa ziara za wawekezaji kila mwezi kati ya Julai na Disemba 2024 kuangalia sekta mbalimbali ikiweka kipaumbele katika sekta ya uchukuzi, fedha, afya, utalii na ujenzi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.