Mkutano wa 16 Wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) la Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika Mei 17, 2024 jijini Arusha Tanzania. Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya ngazi ya watalaam na Mkutano wa Makatibu Wakuu iliyofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 16 Mei 2024.
Mkutano wa SCFCEA ulifanyika sambamba na mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa
Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Mkutano huo alikuwa Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb.), Waziri wa Fedha
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe. Saadah Mkuya (Mb.), Waziri wa Nchi. Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo ulipokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi ya mkutano
wa 15 wa (SCFEA) pamoja na masuala mbalimbali. Aidha, Nchi Wanachama
ziliwasilisha Miongozo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Kaulimbiu za
bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 ambapo Mkutano huo pia ulipitisha Kaulimbiu
ya bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na
kupitisha tarehe 13 Juni 2024 kuwa tarehe ya kusoma bajeti za nchi wanachama.
Vilevile, Mkutano huo ulipitisha Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili
baina ya Nchi Wanachama na Mkataba Kifani wa Kuongoza Majadiliano baina ya Nchi
za EAC na nchi nyingine
Mkutano ukiendelea |
Viongozi wakiwa wamesimama wakati wa ufunguiz wa mkutano |
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia |
Mkutano ukiendelea |
Wajume wakifuatilia mkutano |
Picha ya pamoja |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.