Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba ameagana na
Balozi wa Italia nchini ambaye amemaliza muda wake wa utumishi nchini
hapa nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri Makamba
amemtakia kila la heri Balozi Lambardi na kumpongeza kwa kazi nzuri
aliyoifanya ya kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Italia.
“Uliukuta
uhusiano wa Tanzania na Italia ukiwa katika hali nzuri lakini kwa
nguvu, jitihada na weledi wako umeufanya uhusiano wetu kuwa katika
kiwango cha juu kabisa, tunakupongeza na kukushukuru sana,” alisema
Waziri Makamba.
Naye Balozi Lambardi ameishukuru Wizara na
Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa iliyompatia wakati wote ambao
amekuwa kitekeleza majukumu yake nchini.
“Mhe. Waziri
niwashukuru sana Wizara na hasa Idara ya Ulaya na Amerika kwa
kushirikiana nami na kufanya utendaji wangu kukamilika bila kukwama,
asanteni sana” alisema Balozi Lambardi.
Amesema ana amani kuwa anaondoka nchini huku akiuacha mpango wa Matei ukiwa katika hatua nzuri ya utekelezaji.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.