Friday, June 28, 2024

WAZIRI MAKAMBA ASHIRIKI MKUTANO WA 45 WA KAWAIDA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameongoza ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Kawaida wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika leo tarehe 28 Juni, 2024 jijini Arusha.

 

Mkutano huu pamoja na masuala mengine unapitia na kujadili masuala mbalimbali ya kipaumbele katika ukanda wa EAC ambayo ni, Maendeleo ya Miundombinu, forodha na biashara, masuala ya siasa na kijamii, taarifa ya kamati ya rasilimali watu pamoja na kupokea taarifa ya kamati ya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za jumuiya kwa kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023.

 

Masuala mengine ni pamoja na, jitihada za kubidhaisha Kiswahili kikanda na kimataifa sambamba na taarifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe 7Julai ambayo kikanda yatafanyika nchini Kenya na kuhudhuriwa na Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Kadhalika, mkutano huu pia umejadili na kusisitiza umuhimu wa kuwasilisha michango ya mwaka kwa wakati kutoka kwa nchi zote wanachama ili kuiwezesha Sekretarieti ya EAC kujiendesha na kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya kikanda.

 

Aidha, kupitia mkutano huo Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Veronica Mueni Nduva alijitambulisha kwa Baraza hilo na kueleza nia yake ya kusimamia ustawi wa kikanda katika kukuza uchumi, uvumbuzi, biashara, ajira na amani na usalama  kwa maendeleo endelevu ya wananchi wa EAC.

 

Viongozi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.

 

Mkutano huo umefanyika chini ya Uenyekiti wa Jamhuri ya Sudan Kusini na umehudhuriwa na Nchi zote Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, isipokuwa Somalia imeshiriki kwa njia ya mtandao.


=====================================

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akichangia hoja katika Mkutano wa 45 wa Kawaida wa Barza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika tarehe 28 Juni, 2024 jijini Arusha.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (kulia) pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.) wakifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 28 Juni, 2024 jijini Arusha.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (kati) akifatilia Mkutano wa 45 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa EAC pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Uganda ukifuatilia Baraza la Mawaziri la EAC, aliyekaa kati ni Waziri anayeshughulia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Rebecca Kaganda.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Uganda ukifuatilia Baraza la Mawaziri la EAC, kulia ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Jen. James Kabarebe.
Kulia ni, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Charles Kichere pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya ukaguzi wa hesabu za jumuiya kutoka Nchi za EAC wakikabidhi taarifa ya kamati hiyo kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2023 kwa Mwnyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri, Mhe. Deng Alor Kuol (kushoto).

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Burundi ukifuatilia Baraza la Mawaziri wa EAC.

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ikifuatilia mkutano.

Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Alor Kuol (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Veronica Mueni Nduva  wakiongoza Mkutano wa 45 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa EAC uliofanyika tarehe 28 Juni, 2024 jijini Arusha.

Ujumbe wa kamati ya ukaguzi wa hesabu kutoka nchi za EAC.














Thursday, June 27, 2024

MAKATIBU WAKUU WAKAMILISHA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 45 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC


Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana jijini Arusha kwa kikao cha siku tatu (3) kuanzia tarehe 25 hadi 27 Juni, 2024 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 28 Juni 2024.

 

Mkutano huo wa Makatibu Wakuu ulitanguliwa na mkutano wa wataalam uliofanyika tarehe 22 hadi 24 Juni, 2024 umepokea na kupitia taarifa na mapendekezo yaliyowasilishwa na Mkutano wa wataalam kuhusu masuala mbalimbali  ya kikanda yatakayowasilishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri.

 

Masuala ya kikanda yaliyojadiliwa ni taarifa ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na baraza hilo kwenye vikao vilivyopita, taarifa kuhusu masuala ya forodha na biashara na taarifa ya miundombinu, sekta za uzalishaji, sekta za jamii na masuala ya kisiasa.

 

Taarifa nyingine ni taarifa ya kamati na fedha, taarifa ya kamati ya rasilimali watu, taarifa ya mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 17 Mei, 2024 pamoja na taarifa ya ratiba za matukio ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba, 2024.

 

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa Makatibu Wakuu umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi ambaye ameambatana na, Naibu Katibu Mkuu, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji (Uchumi na Uwekezaji) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Rashid Ali Salim,  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Dkt. John Simbachawene

 

 

Viongozi wengine ni, Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cyrus Kapinga, Kamishna Msaidizi Utafiti kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Bonus Nombo, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uwekezaji Sekta Binafsi Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Bw. Fadhili Chilumba na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, Mhandisi Abdillah Mataka.

======================================


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika

 Mashariki – anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi 

Stephen Mbundi (kulia) akichangia mjadala wakati wa mkutano wa 

Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika  

 tarehe 25 hadi 27 Juni, 2024 jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Katibu 

Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Dkt. John 

Simbachawene.


Naibu Katibu Mkuu, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji 

(Uchumi na Uwekezaji) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Rashid 

Ali Salim na Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera kutoka Ofisi ya Rais – 

Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cyrus 

Kapinga wakifuatilia majadiliano.

Mwenyekiti wa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika 

Mashariki na Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais, anayeshughulikia 

masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, 

Mhe. Beny Gideon Mabor (kati) akiongoza majadiliano ya 

mkutano huo.

Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia 

masuala ya Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Kijamii na Siasa, 

Mhe. Andrea Aguer Ariik Malueth na kulia kwake ni Mwenyekiti wa 

mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka 

Jamhuri ya Sudan Kusini, Bw.  Eulwango Ugo.


Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ikifuatilia mkutano.

Ujumbe kutoka Uganda ukifuatilia mkutano.

Ujumbe kutoka Kenya na Rwanda ukifuatilia mkutano.

Ujumbe kutoka Burundi.



Tuesday, June 25, 2024

BALOZI MBUNDI AONGOZA KIKAO CHA NDANI CHA MAANDALIZI YA MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA EAC


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi ameongoza kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha.


Kikao hicho cha ndani pamoja na masuala mengine kimepitia agenda, taarifa na maagizo mbalimbali yaliyotolewa katika mikutano iliyopita ili kuona hali ya utekelezaji sambamba na kujenga msimamo wa Nchi katika masuala yenye maslahi mapana kwa ustawi wa watanzania na Taifa kwa ujumla.


Mkutano huo wa Makatibu Wakuu wa EAC utafanyika tarehe 26 na 27 Juni, 2024 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Kawaida wa  Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 28 Juni 2024 jijini Arusha. 

=================================

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha.

   Naibu Katibu Mkuu, Afisi ya Rais - Kazi, Uchumi na Uwekezaji (Uchumi na Uwekezaji) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Dkt. John Simbachawene wakifatilia kikao cha ndani wa ujumbe wa Tanzania kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha. 


Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cyrus Kapinga akifatilia kikao.

   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, Mhandisi Abdillah Mataka akiwasilisha taarifa ya mkutano wa Maafisa Waandamizi uliomalizika leo tarehe 25 Juni, 2024.

=======================

Maafisa waandamizi wakifatilia kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu kiliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2024.










Monday, June 24, 2024

WIZARA YA MAMBO YA NJE ILIVYOSHIRIKI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amesema maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 23 Juni kila mwaka yanalenga kuhamasisha uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika utumishi wa umma barani Afrika

Waziri Mkuu alisema hayo wakati wa hafla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na ufunguzi wa mifumo ya kielekitroniki ya uwajibikaji katika utumishi wa umma (E-UTUMISHI) iliyofanyika juni 23, 2024 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Taasisi za Umma ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ilishiriki maadhimisho hayo zilielekezwa kuhakikisha kuwa zinajiunga kwenye mifumo hiyo na kuwa na mpango endelevu wa kuwaelimisha watumishi namna ya kuitumia.

Mifumo hiyo ni pamoja na mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS); Mfumo wa Utumishi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma ((PEPMIS/PIPMIS), Mfumo wa Tathmini ya Rasilimaliwatu (HRA) na Mfumo wa Kushughulikia  Mrejesho wa Wananchi  kuhusu Huduma Zinazotolewa na Serikali (e-MREJESHO).

Amesema mifumo hiyo ni muhimu kwa kuwa inarahisisha na kuharikisha huduma kwa wananchi pamoja na kuondoa kero kama vile za rushwa na urasimu. 

Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla kuchangamkia mifumo hiyo ambayo imeunganishwa na taasisi nyingine kama za huduma za kifedha, mifuko ya pensheni na Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho.

Waziri Mkuu aliwapongeza wabunifu wa mifumo hiyo ambao wote ni Watanzania kwa kubuni mifumo yenye tija na ubora mkubwa ambayo imetambuliwa na taasisi ya umoja wa mataifa ya “United Nations Public Services Awards”.

Waziri Mkuu alihitimisha hotuba yake kwa kuagiza kila Mkuu wa taasisi aweke mipango ya usimamizi na uongozi wa mifumo hiyo ili iweze kutumika kwa ufanisi katika ngazi ya taasisi yake; taasisi za umma zihakikishe usalama wa takwimu na taarifa zinazowekwa kwenye mifumo hiyo. Alisema mifumo hiyo ina taarifa muhimu na nyeti, hivyo ni muhimu kuhakikisha taarifa hizo zinalindwa ipasavyo ili kuepuka uhalifu wa kimtandao pamoja na kutoa mafunzo na kuhamasisha matumizi ya mifumo hiyo ambayo ni migeni kwa watumishi. 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2024.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo (Wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea Banda la  Wizara wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2024.

Mwananchi akipata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa diplomasia ya Uchumi alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2024.
Mwananchi akihudumiwa alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2024.

Wananchi wakihudumiwa walipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2024.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifafanua masuala mbalimbali kuhusu utendaji wa Wizara hiyo kwa Mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2024.

 

MAANDALIZI YA MKUTANO WA 45 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC YAENDELEA JIJINI ARUSHA

 

Maandalizi ya Mkutano wa Kawaida wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yanaendelea jijini Arusha katika kikao ngazi ya Maafisa Waandamizi.

 

Mkutano huo wa Mawaziri utafanyika tarehe 28 Juni, 2024 na unatanguliwa na vikao vya awali vya maandalizi ambavyo ni; Kikao cha Maafisa Waandamizi kilichoanza tarehe 22 Juni 2024 na kitahitimishwa leo tarehe 24 Juni, 2024 na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 25 hadi 27 Juni 2024.

 

Pamoja na masuala mengine mkutano huo utapitia na kujadili taarifa mbalimbali kama ifuatavyo,  taarifa ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na baraza hilo kwenye vikao vilivyopita, taarifa kuhusu masuala ya forodha na biashara na taarifa ya miundombinu, sekta za uzalishaji, sekta za jamii na masuala ya kisiasa.

 

Taarifa nyingine ni, taarifa ya kamati na fedha na rasilimali watu, taarifa ya mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 17 Mei, 2024 pamoja na taarifa ya kalenda ya matukio ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba, 2024.

 

Mkutano huu unahudhuriwa na nchi zote wanachama ikiwemo, Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania akiwa mwenyeji, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Somalia imeshiriki kwa njia ya mtandao.

 

=============================

Meza kuu; Kushoto ni Mwenyekiti wa kikao cha Maafisa Waandamizi, Bw. Eulwango Ugo kutoka Jamhuri ya Sudan Kusini akiongoza kikao cha Maafisa Waandamizi na pembeni ni Mkuu wa masuala ya Sheria kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika mashariki(EAC), Dkt. Anthony Kafumbe.

Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilson Gwoma wakifuatilia majadiliano.

Maafisa kutoka Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Maafisa Waandamizi wa EAC, kutoka kulia ni Dkt. Elias Bagumhe na Bw. Othman Chanzi.

 Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Jasinta Mboneka na Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abel Maganya wakifuatilia majadiliano.

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ukifuatilia majadiliano.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kenya.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Rwanda.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Burundi.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Uganda.


Thursday, June 20, 2024

RAIS WA GUINEA BISSAU KUFANYA ZIARA RASMI NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akitangaza rasmi ziara ya Rais wa Guinea Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaro itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Juni 2024. Ziara hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Guinea Bissau. Balozi Shelukindo ametangaza ziara wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofamyika jijini Dar es Salaam tarehe 20 Juni 2024

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Sakila (kulia) akifuatilia Mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Shelukindo (hayupo pichani) na Wandishi wa Habari akitangaza kuhusu ziara ya Rais wa Guinea Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embalo itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Juni 2024

Mkutano ukiendelea


 

Wednesday, June 19, 2024

WIZARA YA MAMBO YA NJE NI KATI YA WIZARA 14 NA TAASISI 60 ZINAZOSHIRIKI MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kujenga Kituo cha Kimataifa cha Mikutano jijini Dodoma kufuatia jiji hilo kukua kwa kasi na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa, yenye ubora wa hali ya juu.

Ushauri huo umetolewa leo Juni 19, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) alipotembelea Banda la Wizara katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda alimwambia Mhe. Waziri Simbachawene kuwa Wizara kwa sasa, kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) inaendelea na mchakato wa kujenga Kituo kipya cha Mikutano jijini Arusha ambacho kinatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa APIMONDIA Unaohusu ufugaji wa nyuki unaotarajiwa kufanyika Arusha mwaka 2027 na utahusisha wadau zaidi ya 6000.

 

Waziri Simbachawene ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo alitoa wito kwa watumishi na wananchi kwa ujumla kuwa na mwamko wa kutumia mifumo ya TEHAMA inayoanzishwa na taasisi za umma kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma na kuondoa ukiritimba na urasimu.

 

“Taasisi za umma takribani zote nchini zina mifumo ya TEHAMA ya kutoa huduma lakini mwamko kwa wananchi bado sio mzuri wa kutumia mifumo hiyo ambayo lengo lake ni kuharakisha huduma na kuwaondolea usumbufu wananchi” Waziri Simbachawene alisema.

 

Waziri Simbachawene alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ambayo yatafungwa tarehe 23 Juni 2024 ili waweze kupata huduma za papo kwa papo na taasisi zinazoshiriki ikiwa ni pamoja na kupata hati za viwanja, vitambulisho vya taifa na kupima afya.

 

Wizara na taasisi zake za AICC, Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na Mpango wa Afrika Kujitathimini Kiutawala Bora (APRM-Tanzania) ni kati ya Wizara 14 na taasisi 60 zinazoshiriki maonesho hayo. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda (kushoto) alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipokea zawadi ya Diary na Calendar kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi zake wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda akipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Afisa kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Nyanzobe Hemed akihudumia wananchi waliojitokeza katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma