Wednesday, June 19, 2024

WIZARA YA MAMBO YA NJE NI KATI YA WIZARA 14 NA TAASISI 60 ZINAZOSHIRIKI MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kujenga Kituo cha Kimataifa cha Mikutano jijini Dodoma kufuatia jiji hilo kukua kwa kasi na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa, yenye ubora wa hali ya juu.

Ushauri huo umetolewa leo Juni 19, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) alipotembelea Banda la Wizara katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda alimwambia Mhe. Waziri Simbachawene kuwa Wizara kwa sasa, kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) inaendelea na mchakato wa kujenga Kituo kipya cha Mikutano jijini Arusha ambacho kinatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa APIMONDIA Unaohusu ufugaji wa nyuki unaotarajiwa kufanyika Arusha mwaka 2027 na utahusisha wadau zaidi ya 6000.

 

Waziri Simbachawene ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo alitoa wito kwa watumishi na wananchi kwa ujumla kuwa na mwamko wa kutumia mifumo ya TEHAMA inayoanzishwa na taasisi za umma kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma na kuondoa ukiritimba na urasimu.

 

“Taasisi za umma takribani zote nchini zina mifumo ya TEHAMA ya kutoa huduma lakini mwamko kwa wananchi bado sio mzuri wa kutumia mifumo hiyo ambayo lengo lake ni kuharakisha huduma na kuwaondolea usumbufu wananchi” Waziri Simbachawene alisema.

 

Waziri Simbachawene alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ambayo yatafungwa tarehe 23 Juni 2024 ili waweze kupata huduma za papo kwa papo na taasisi zinazoshiriki ikiwa ni pamoja na kupata hati za viwanja, vitambulisho vya taifa na kupima afya.

 

Wizara na taasisi zake za AICC, Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na Mpango wa Afrika Kujitathimini Kiutawala Bora (APRM-Tanzania) ni kati ya Wizara 14 na taasisi 60 zinazoshiriki maonesho hayo. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda (kushoto) alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipokea zawadi ya Diary na Calendar kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi zake wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda akipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Afisa kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Nyanzobe Hemed akihudumia wananchi waliojitokeza katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma


 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.