Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameanza kazi rasmi katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kombo ameanza majukumu hayo muda mfupi baada ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri Mhe. January Makamba (Mb).
Makabidhiano hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Mawaziri ambao waliteuliwa pamoja, Mhe. Cosato Chumi na Mhe. Dennis Londo
Mhe. Waziri katika siku yake ya kwanza amekutana na kufanya mazungumzo na Mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile.
Aidha, Mhe. Waziri amekutana na baadhi ya Wakurugenzi waliopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutekeleza majukumu
Saturday, July 27, 2024
WAZIRI KOMBO AANZA KAZI RASMI
Friday, July 26, 2024
BALOZI KOMBO NA MANAIBU WAKE WAPOKELEWA KATIKA OFİSİ NDOGO ZA WIZARA DSM
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud
Thabit Kombo amewasili na kupokelewa katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam akitokea Ikulu ya Dar es Salaam baada ya kuapishwa
kuwa Waziri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Katika mpokezi hayo, Mhe. Balozi Kombo
aliiambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Cosato Chumi na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe.
Dennis Lazaro Londo na kulakiwa kwa bashasha na viongozi na Watumishi
wa Wizara waliokusanyika katika Ofisi ndogo, Dar Es Salaam.
Mhe.
Balozi Kombo pamoja na Naibu Mawaziri, Mhe. Londo na Mhe. Chumi
waliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan kushika nyadhifa hizo katika mabadiliko madogo ya Baraza
la Mawaziri yaliyofanyika Julai 21, 2024
RAIS SAMIA AWAAPISHA MHE. BALOZI KOMBO NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR ES SALAAM
Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akiapa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu Dar es Salaam, Julai 26, 2024 |
Mhe. Dennis Lazaro Londo akiapa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Masharika, Ikulu Dar es Salaam, Julai 26, 2024 |
Mhe. Cosato Chumi akiapa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu Dar es Salaam, Julai 26, 2024 |
Mawaziri na Manaibu Waziri Wakiapa kiapo cha Uadilifu baada ya kuapishwa na Mhe. Rais kushika nyadhifa hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2024. |
Mawaziri na Manaibu Waziri wakisaini Hati ya kiapo cha Uadilifu baada ya kula kiapo hicho na kuapishwa na Mhe. Rais kushika nyadhifa hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2024. |
Thursday, July 25, 2024
DKT. TULIA AMUAPISHA BALOZI MAHMOUD THABIT KOMBO KUWA MBUNGE
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson
amemuapisha Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika hafla ndogo iliyofanyika Ofisi Ndogo za
Bunge jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai,2024.
Hafla hiyo ya
uapisho imehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.
Dkt. Stergomena Tax, Naibu Waziri Mteule wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe.
Dennis Lazaro Londo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Naibu Katibu Mkuu
Balozi Said Shaib Mussa na watendaji wengine wa Ofisi ya Bunge.
Tarehe
21 Julai, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan alimteua Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo kuwa Mbunge na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Rais pia aliwateua Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mhe. Cosato David Chumi (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje. Waziri.
Mhe. Balozi Kombo na Manaibu Waziri wateule wataapishwa tarehe 26 Julai, 2024 Ikulu jijini Dar es salaam.
Wednesday, July 24, 2024
TANZANIA-COMORO ZASAINI HATI NNE ZA MAKUBALIANO
Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro wakifurahia jambo |
Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika tarehe 24 Julai,2024 ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
Picha ya pamoja |
DKT. TAX AKUTANA NA KAIMU NAIBU WAZIRI WA MAREKANI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb), amekutana kwa mazungumzo na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho Dkt. Tax amemuhakikishia Mhe. Bass kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Marekani katika masuala yenye manufaa kwa nchi hizi mbili na wananchi wake.
Amesema ziara ya Mhe. Bass nchini ni ushahidi wa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili huku ikonesha umuhimu mkubwa katika kuendelea kudumisha na kuimarisha maelewano, ushirikiano na urafiki kati ya Tanzania na Marekani na kuongeza kuwa kwa miaka mingi kumekuwa na majadiliano ya wazi kwa ajili ya kujenga na kuweka misingi ya ushirikiano madhubuti kati ya Tanzania na Marekani.
“Nina Imani kuwa kupitia ushirikiano na uhusiano wetu sio kwamba tutakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja bali pia tutanufaika na fursa zilizopo mbele yetu ili kuchochea ukuaji na ustawi wa pamoja, alisema Dkt. Tax.
Naye Mhe. Bass akizungumza katika kikao hicho amesema ziara yake nchini ina lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Tanzania na kuahidi kuwa Marekani inaiona Tanzania kama mdau wa kimkakati katika ushirikiano wa maendeleo.
Ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya Marekani na kuongeza kuwa ni matarajio yake kuwa kupitia majadiliano mbalimbali ambayo yemekuwa yakifanyika yatasaidia nchi yake kuibua kwa undani maeneo muhimu ambayo Serikali ya Tanzania inahitaji kuendelea ushirikiana na Marekani.
Tanzania na Marekani zimekuwa zikishirikina katika nyanja za afya kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la USAID, elimu, kilimo, biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama.