DKT. TULIA AMUAPISHA BALOZI MAHMOUD THABIT KOMBO KUWA MBUNGE
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson
amemuapisha Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika hafla ndogo iliyofanyika Ofisi Ndogo za
Bunge jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai,2024.
Hafla hiyo ya
uapisho imehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.
Dkt. Stergomena Tax, Naibu Waziri Mteule wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe.
Dennis Lazaro Londo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Naibu Katibu Mkuu
Balozi Said Shaib Mussa na watendaji wengine wa Ofisi ya Bunge. Tarehe
21 Julai, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan alimteua Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo kuwa Mbunge na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Rais pia
aliwateua Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb) kuwa Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mashariki na Mhe. Cosato David Chumi (Mb) kuwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje. Waziri.
Mhe. Balozi Kombo na Manaibu
Waziri wateule wataapishwa tarehe 26 Julai, 2024 Ikulu jijini Dar es
salaam.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.