Friday, October 11, 2024

BALOZI SHELUKINDO AFUNGA MAFUNZO


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifunga mafunzo ya siku nne (4) ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara hiyo yaliyofanyika jijini Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo leo tarehe 11 Oktoba 2024 amefunga rasmi mafunzo ya siku nne (4) ya mawasiliano ya kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara hiyo yaliyofanyika jijini Dodoma.

Mafunzo hayo yaliyotolewa na timu ya Mabalozi Wastaafu sita (6) akiwemo Balozi Bertha Semu-Somi, Balozi Mohammed Maundi, Balozi Begum Taji, Balozi Peter Kalaghe, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Mohamed Hamza yalijikita katika kujenga ubunifu na uelewa katika mawasiliano ya kidiplomasia na mafunzo ya nadharia na vitendo ya uandishi wa taarifa za kidiplomasia.
Katibu wa Mabalozi Wastaafu, Balozi Bertha Semu Somi akifafanua jambo kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akimkaribisha Katibu Mkuu Balozi Dkt. Samwel Shelukindo kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara hiyo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Afisa Mambo ya Nje Bi. Symphrosa Chacha akitoa neno la shukrani kwa waandaaji na wawezeshaji wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Katibu wa Mabalozi Wastaafu, Balozi Bertha Semu Somi wakijadili jambo
Mafunzo ya kiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.