Rais Mstaafu wa Zanzibar na
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume ameendelea
kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa
kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Mhe. Dkt. Karume kwa nyakati tofauti leo tarehe 05 Oktoba 2024
jijini Maputo, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri la Msumbiji, Mchungaji Augusto Pedro na Mkurugenzi wa Kituo cha
Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD), Prof. Adriano Nuvunga.
Katika mazungumzo yake na
viongozi hao, Mhe. Dkt. Karume pamoja na mambo mengine aliwaeleza lengo la
Misheni hiyo ya SADC kuwa ni kuangalia uchaguzi kwa mujibu wa kanuni na
miongozo ya uchaguzi ya SADC iliyorekebishwa mwaka 2021 inayozingatia misingi
ya haki, usawa na demokrasia.
Ujumbe wa Mhe. Dkt. Karume
kwenye mikutano hiyo uliwajumuisha
Wajumbe wa Troika kutoka Tanzania, Zambia na Malawi, Sekretarieti ya SADC
akiwemo Mkurugenzi wa Organ , Prof. Kula Ishmael Theletsane na
Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa masuala
ya Uchaguzi la SADC (SEAC). Wajumbe wa
Troika kutoka Tanzania walioshiriki ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na
Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema.
Vilevile, Mhe. Dkt. Karume
amepokea taarifa kutoka kwenye Kamati ya Uandishi ya Misheni hiyo kuhusu utekelezaji
wa masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa kutoka kwa waangalizi wa
SADC ambao walisambazwa kwenye majimbo 11 ya uchaguzi nchini humo tangu tarehe
03 Oktoba 2024.
Mhe. Dkt. Karume kwa nafasi yake ya Mkuu wa Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC ameendelea kukutana na viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa uchaguzi ambapo hadi sasa amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Mabalozi wa Nchi za SADC waliopo Msumbiji, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Kamishna Msidizi wa Jeshi la Polisi la Msumbiji na Mgombea urais wa Chama Tawala cha FRELIMO, Mhe. Daniel Francisco Chapo.
Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji, Mchungaji Augusto Pedro akizungumza na Mkuu wa Misheni ya SADC ya uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Karume (hayupo pichani) |
Mhe. Dkt. Karume akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD), Prof. Adriano Nuvunga katika mkutano uliofanyika jijini Maputo tarehe 5 Oktoba 2024 |
Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Balozi wa Malawi nchini Msumbiji, Mhe. Wezi Moyo akichangia jambo. Kushoto ni Mjumbe wa Troika kutoka Zambia, Bw. Lubasi |
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri naye akichangia jambo |
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Taarifa ya Misheni ya SADC, Bi. Shazma Msuya akitoa taarifa kwa Mkuu wa Misheni ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Karume (hayupo pichani) |
Bi. Msuya akiwasilisha taarifa kwa Mkuu wa Misheni, Mhe. Dkt. Karume |
Uwasiishaji taarifa ya Misheni ukiendelea |
Mhe. Dkt. Karume akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji baada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Karume akiagana na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji mara baada ya mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Karume akiagana na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD), Prof. Adriano Nuvunga baada ya mazungumzo yao |
Picha ya pamoja |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.