Tuesday, November 26, 2024

TANZANIA YAPONGEZWA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA EAC

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Veronica Nduva  ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipa uzito wa kipekee agenda ya maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo kilele chake ni tarehe 30 Novemba 2024.

 

Mhe. Nduva ametoa pongezi hizo wakati akitoa taarifa ya masuala mbalimbali ya kiutendaji kuhusu Sekretarieti ya EAC ikiwa ni pamoja na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya maadhimisho hayo kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Nchi Wanachama kinachoendelea jijini Arusha.

 

Amesema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mkoa wa Arusha na kwa kushirikiana na Sekretarieti ya EAC imefanikisha kwa kiasi kikubwa kuandaa shughuli mbalimbali kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na  kuandaa tamasha la maonesho ya barabarani, maonesho ya utamaduni na zoezi la upandaji miti.

 

Kuhusu matukio muhimu kwenye maadhimisho hayo, Mhe. Nduva amesema zipo program za pembezoni za Ngazi ya Juu kuhusu maadhimisho hayo zitakazowahusisha Wakuu wa Nchi wa EAC pamoja na Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Wakuu hao wa Nchi utakaofanyika tarehe 29 na 30 Novemba 2024.

 

Amesema patakuwa  na  mijadala mbalimbali yenye mada kuhusu masuala ya  Biashara na Uwekezaji katika Jumuiya,  masuala ya Kidigitali na Amani na Usalama pamoja na tukio la upandaji miti kama kumbukumbu nzuri ya maadhimisho hayo.

 

Pia ameendelea kuzihamasisha Nchi Wanachama kushiriki katika maadhimisho hayo muhimu kwao ambayo ameyataja kama moja ya kipimo cha mafanikio ya Jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 1999.

 

“Kama Nchi Wanachama tunajivunia miaka 25 ya Jumuiya imara ambayo ni nusu karne, sina uhakika wengi wetu tuliopo kwenye chumba hiki tutakuwa wapi tunapoitafuta miaka mingine 25 ya Jubilee ya Jumuiya. Hivyo, nawaomba tuungane pamoja kuanzia tarehe 29 hadi 30 Novemba 2024 kusherehekea miaka hii 25 ya mafanikio ya Jumuiya yetu”, alisema Mhe. Nduva.

 

Mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulisainiwa jijini Arusha tarehe 30 Novemba 1999. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Tunasherehekea miaka 25 ya Mtangamanao wa Kikanda na Maendeleo”.

 

Mkutano wa Makatibu Wakuu wa EAC kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki umemalizika leo tarehe 26 Novemba 2024 ambapo Mkutano wa Baraza hilo utafanyika tarehe 28 Novemba 2024. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi.

 

Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 na 26 Novemba 2024 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Eliakim Maswi na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji , Dkt. Tausi Kida. 
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bi. Veronica Nduva akizungumza wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu. Pamoja na mambo mengine aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kwenye maandalizi ya maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah akishiriki Mkutano wa wa Makatibu Wakuu wa EAC
Sehemu ya ujumbe wa Rwanda wakishirki mkutano
Mjumbe wa Somalia akiwa kwenye Mkutano
Ujumbe wa Uganda ukishiriki mkutano
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Chiku Kiguhe akishiriki Mkutano pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Miundombini ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara hiyo, Bw. Abdillah Mataka
Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mioango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justine Kisoka akiwa na Wakurugenzi wengine Bw. Mataka na Bi. Kiguhe
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano
Mkutano ukiendelea


Sunday, November 24, 2024

WAZIRI KOMBO: TANZANIA ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KULETA AMANI NA USALAMA UKANDA WA MAZIWA MAKUU


Waziri Mambo ya Nje na Uashirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024. 

Waziri Mambo ya Nje na Uashirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa Tanzania ikiwa ni mwasisi wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Mkuu (ICGLR) itaendelea kushirikiana na nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo na Jumuiya ya Kimataifa katika juhudi za kutafuta amani ya kudumu kwenye ukanda huo. 

Waziri Kombo ameeleza hayo alipozungumza katika Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024. 

Akizungumzia kuhusu msimamamo, mchango na nafasi ya Tanzania katika kufatua amani na usalama kwenye ukanda wa Maziwa Makuu Waziri Kombo ameeleza kuwa, Tanzania chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itafanya kazi bila kuchoka kwa kushirikiana na nchi wanachama na Jumuiya ya Kimataifa kutatua migogoro iliyopo ili kuwa na ukanda wenye amani, ustawi na ustahimilivu.

“Kama mwanachama mwanzilishi wa ICGLR, Tanzania inaamini kuwa kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia na kuimarishwa kwa utulivu kutaongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi ya watu wetu katika Ukanda wa Maziwa Makuu” Ameeleza Waziri Kombo. 

Aidha, Waziri Kombo licha ya kueleza utayari wa Tanzania katika kuendelea kushirikiana na wadau katika kurejesha amani na usalama kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, ametoa wito kwa nchi wanachama kuhakikisha kuwa ushawishi wa washirika wa maendeleo hauathiri utendaji na ufanisi wa mifumo iliyowekwa ikiwemo Mfumo wa Tahadhari ya Mapema na Majibu ya Migogoro wa ICGLR (ICGLR Conflict Early Warning and Response Systems).

Vilevile, amesisitiza umuhimu wa nchi Wanachama kuheshimu na kutimiza wajibu wake wa kuchangia fedha kwa Sekretarieti, ikiwa ni ishara ya mshikamano na juhudi za pamoja, katika kuhakisha Jumuiya inatekeleza mipango na mikakati inayojiwekea ili kufikia matarajio ya kuwa na ukuanda wenye Usalama, Utulivu, na Maendeleo endelevu. 

Pia ametumia fursa hiyo kuitaka Sekretareti ya ICGLR kuzingatia matumizi mazuri na usimamizi mzuri wa fedha kwa manufaa ya kanda. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Balozi Téte António akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ameleeza ameeleza kuridhishwa kwake na mazungumzo yanayo endelea yakilenga kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na DRC. 

Aliendelea kutoa wito kwa nchi wanachama kwa umoja wao kuendelea kushughulikia changamoto zinazotishia amani, usalama, na hali ya kibinadamu katika Jamhuri ya Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, na ghasia zinazoendelea katika Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote 12 Wanachama wa Maziwa Makuu na Mjumbe Maalumu kutoka Umoja wa Mataifa anayesimamia Ukanda wa Maziwa Mkuu Balozi Huang Xia.
Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Mhe. Musalia Mudavadi Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya (Prime Cabinet Secretary) wafurahia jambo pembezoni mwa mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Balozi wa Tanzania nchini Angola mwenye makazi yake nchini Zambia Mhe. Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule akifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliokuwa ukiendelea jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Balozi Téte António kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Picha ya pamoja
Mkutano ukiendelea 






MHE. MAKINDA AKUTANA NA DKT. SPECIOZA WANDIRE-KAZIBWE MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA UMOJA WA AFRIKA

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Namibia kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM), Mhe. Anne Makinda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AUEOM) na Makamu wa Rais wa Zamani wa Uganda Dkt. Specioza Wandire-Kazibwe, tarehe 24 Novemba 2024, jijini Windhoek Namibia.

Katika kikao hicho Mhe, Makinda aliambatana na mjumbe wa Organ Troika na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa pamoja na na mwakilishi wa Secretarieti ya SADC.

Akizungumza na Dkt. Wandire-Kazibwe kuhusu maendeleo ya ufuatiliaji wa Uchaguzi Mkuu wa Namibia, Mhe. Makinda amesema SEOM imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi na kuzungumzia pamoja na mambo mengine, hali ya ulinzi na usalama, siasa na maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao katika ujumla wake.

Naye Mkuu wa AUEOM Dkt. Wandire-Kazibwe, amezitaka taasisi za akademia na za utafiti katika nchi wanachama wa SADC zikiwemo Vyuo, kupanua maeneo ya kufanyia utafiti katika siku sijazo na kujumuisha maeneo ya siasa, uchumi, demokrasia na masuala yahahusu uchaguzi; ili matokeo ya tafiti hizo yatumike kuimarisha mipango ya kisiasa, kiuchumi na kijamii pamoja na kuwezesha kufanyika kwa maboresho sera, ilani za vyama vya siasa, sheria, na miongozo mbalimbali inayohusu ukuaji uchumi wa mataifa.

Katika tukio lingine , Mhe. Makinda pia alikutana na Kiongozi taasisi inayosimamia uendeshaji wa Waandishi wa Habari nchini Namibia (Media Ambudsman of Namibia) ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Namibia Dkt. John Nakuta.

Akizungumza kuhusu wajibu wa vyombo vya habari, Dkt. Nkuta amesema wakati Namibia inajiandaa kwa uchaguzi mkuu, vyombo vya habari vya Serikali na binafsi vinapaswa kuzingatia haki, usawa, na sheria za nchi katika kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kusema ukweli wakati wote. 

Na kuongeza kuwa wakifanya hivyo watasaidia kuwapa wagombea na wananchi haki yao ya msingi ya kupata habari.

Wananchi wapatao 1,449,569 wanaripotiwa kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo, yenye wakazi zaidi ya milioni tatu.


 

Friday, November 22, 2024

VIKAO KUANDAA MKUTANO WA 46 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA EAC VYAANZA JIJINI ARUSHA

Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Ngazi ya Wataalam umeanza jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano huo utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024.

 

Pamoja na mambo mengine, mkutano wa wataalam unajadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri.

 

Taarifa zilizopokelewa na kujadiliwa ni pamoja na Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya awali ya Baraza la Mawaziri; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu masuala Forodha, Biashara na masuala ya kifedha; Taarifa kuhusu Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Sekta za Kijamii na masuala ya Kisiasa; Taarifa kuhusu masuala Fedha na Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya.

 

Mkutano wa Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji Janabi kwa niaba ya Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao

 

Mkutano huu wa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 ukifuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 26 Novemba 2024 na  tarehe 27 na 28 Novemba 2024 utafanyika Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri ambao utapokea agenda mbalimbali kutoka kwa Makatibu Wakuu .

 

Agenda zitakazojadiliwa katika Baraza la Mawaziri zitawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2024 kwa ajili ya kupitishwa na kuridhiwa kwa utekelezaji.

 

Nchi nane Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda zinashiriki mkutano huo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji Janabi akiongoza kikao kwa niaba ya Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao. Kikao hicho cha ngazi ya wataalam  kimefanyika jijini Arusha kuandaa Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024. Kikao cha Wataalaam kitafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu mnamo tarehe 26 Novemba 2024.M

Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Benjamin Mwesiga akichangia jambo wakati wa kikao cha Wataalam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abdilah Mataka akifuatilia kikao
Sehemu ya ujumbe wa Burundi wakishiriki Mkutano wa Wataalam
Ujumbe wa Kenya

Ujumbe wa Somalia

Ujumbe wa Uganda

Sehemu ya Wajumbe wakishiriki kikao cha wataalam

Sehemu nyingine ya wajumbe wakati wa kikao

Wajumbe wakishiriki kikao

Ujumbe wa Tanzania wakishiriki kikao

Kikao kikiendelea

Wajumbe wakati wa kikao



Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea